Kufuatia Hatua Ya Tangazo La Isis Kutangaza Dola Ya Khilafah

ﺑﺴﻢ ﷲ ﺍﻟﺮﺣﻤﻦ ﺍﻟﺮﺣﻴﻢ

Kwa akina kaka na akina dada zetu waliotuma masuala kuhusu hatua ya taasisi ya ISIS kutangaza  kuasisiwa kwa dola ya Khilafah. Mtaniwia radhi sana kwa kutotaja majina yenu, kwa kuwa orodha  ya majina yenu ni ndefu. …

Assalamu alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu,

Tumeshatuma majibu ya hili awali, hata hivyo tunajibu tena hivi:

Wapendwa ndugu zangu na dada zangu,

1.Hakika kikundi chochote kinachokusudia kutangaza Khilafah pahala popote pale basi ni wajibu juu yake kufuata njia ya Mtume (saaw) katika hilo. Na miongoni mwa mambo hayo ni kikundi hicho kuwa na mamlaka kamili ya wazi katika eneo hilo, wakiwa na udhibiti wa usalama wa ndani na wa nje wa eneo hilo. Na pia eneo hilo ambalo inatangazwa Khilafah liwe na vigezo vya dola. … Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Mtume (saaw) pindi aliposimamisha dola ya Kiislamu Madina: Hakika mamlaka yalikuwa kwa Mtume (saaw) na amani ya ndani na nje ikisimamiwa na utawala wa Kiislamu, na dola ilikuwa na vigezo  katika eneo lote.

2. Kikundi ambacho kimetangaza Khilafah hakina mamlaka sio ndani ya Syria wala Iraq, na hakina uwezo wa kudhamini usalama na amani sio ndani wala nje, bali kubwa zaidi wamempa bay’ah mtu ambaye hana hata uwezo wa kuonekena na kujitangaza hadharani bali ameendelea kuwa mwenye kujificha kama alivyokuwa kabla ya kutangaza dola! Na hili ni kinyume kabisa na alivyofanya Mtume (saaw), aliruhusiwa Mtume (saaw) kabla ya dola kujificha ndani ya pango la Thaur lakini baada ya kusimamisha dola alikuwa anasimamia mambo ya ummah, akiongoza jeshi, kutatua mizozo baina ya wagomvi na akituma na kupokea  mabalozi na wajumbe bila ya kificho. Hivyo, bila ya shaka hali ilitofautika baina ya kipindi cha kuwa hana dola, na baada ya kupata dola… Basi kikundi hicho kutangaza  Khilafah ni upuuzi na wala hakina dhamana  wala uzito wowote. Kikundi hicho ni sawa na waliokwisha kitangulia awali kutangaza Khilafah isiyokuwa na uhalisia katika kuasisiwa kwake wala vigezo bali kufurahisha nafsi na tamaa zao tu, na huyu aliyejitangaza Khalifah ni kama wale wanaojitangaza kuwa ni Mahd… Bila ya kuwa na vigezo, mamlaka/ nguvu, dhamana ya usalama wala udhibiti wa amani….!

  1. Hakika Khilafah ni dola yenye uzito na unyeti mkubwa, sharia imebainisha njia ya kusimama kwake na namna itakavyovua hukmu zake katika utawala, siasa, uchumi, na mahusiano ya kimataifa… na si tangazo tu la jina la kutangazwa katika tovuti au kuzagaa katika mitandao (ya kijamii na tovuti) na vyombo vya habari  kwa kusomwa, kusikika au kutazamwa. Bali litakuwa ni tukio kubwa litakalotikisa dunia, huku mizizi yake imekita ardhini na utawala wake utahifadhi amani ya ndani na nje katika ardhi hiyo, na itatawalisha Uislamu ndani ya nchi litakapoasisiwa na kuubeba ulinganizi wa Uislamu nje kwa da’wa na jihadi…
  2. Hakika tangazo lilotokea ni upuzi na kamwe halitozidisha au kupunguza muundo wa dola. Kikundi kilichotangaza hili ni harakati ya wanamgambo wa kijeshi kabla na baada ya tangazo. Na mfano wake ni kama vilivyo vikundi vyengine vya kisilaha vinavyopigana na vikundi vyengine na pia kupigana na serikali. Bila ya vikundi hivi  kuwa na utawala ndani ya Syria au Iraq au zote mbili. Lau kama vikundi hivi kikiwemo hichi cha (ISIS) vingekuwa na utawala wenye uzito katika sehemu husika iliyotimiza vigezo vya dola na vikatangaza kusimamisha Khilafah na kuanza kutawalisha sheria basi vingestahiki kufanyiwa uchunguzi kwa makini ili kuangaliwa je Khilafah walioisimamisha ina sifa za kisheria? Hapo (kama iko sawa) ingefuatwa dola hiyo kwani kusimamisha Khilafaha ni faradhi kwa Waislamu na si faradhi kwa Hizb ut-Tahrir pekee. Yeyote atakaye isimamisha kwa kutimiza vigezo vyake atafuatwa… Bali mambo si hivyo kwani vyote ni vikundi vya kisilaha yaani “wanamgambo” na miongoni mwao ni ISIS. Hakuna vigezo vya dola wala utawala, wala usalama na amani katika ardhi, hivyo kutangaza kwao (ISIS) Khilafah ni upuuzi ambao hauna hadhi wala kustahiki  kufanyiwa hata uchambuzi wa uhalisia wake kwani  suala lake liko wazi  shahir dhahir.
  3. Hata hivyo jambo linalostahiki kuchunguzwa na kufanyiwa ufafanuzi ni sura mbaya inayoweza kujitokeza kutokana na tangazo hili kuleta athari mbaya kwa watu wasiokuwa na uwezo mkubwa wa kupima mambo (kisheria) ikasababisha wapoteze fikra ya ubora wa Khilafah na umuhimu wake mkubwa, ukaporomoka ufahamu mzuri wa Khilafah  na kugeuka kana kwamba ni mchezo wa kutoa joto liliojaa vifuani mwa baadhi ya watu kutokana na misukukosuko. Ikawa kwa kila anayejisikia anasimama katika uwanja au kijiji kisha akatangaza kuwa yeye ni Khalifah.  Kisha anapotea na kudhani kuwa amefanya  jambo jema.  Basi hali hiyo itapoteza umuhimu, unyeti na ukubwa wa Khilafah katika nyoyo za hawa wasio wajuzi sana wa mambo na kubakia ni jina zuri tu kwa yeyote anayetaka kujipachika bila ya kuwa na vigezo stahiki… Hili ndilo jambo linalostahiki kuchunguzwa na kufanyiwa uchambuzi hasa katika wakati huu ambao kusimama kwa Khilafah kumekaribia kuliko ilivyokuwa hapo awali, na wamekuwa Waislamu wakisubiri kwa shauku kubwa sana na wao wanaona Hizb ut-Tahrir imeambatana na sera ya Mtume (saaw) katika usimamishaji wake ndani ya Madina… Kisha wanaona maingiliano makubwa yaliohai na yenye kuathiri baina ya Hizb na Umma ambao unaounga mkono, Waislamu wakafahamu kutokamana na maingiliano haya maana ya udugu katika Uislamu na wanaiombea Hizb kheri ipate mafanikio katika kusimamisha Khilafah na usimamizi mzuri wa mambo ya Ummah. Na Khilafah iwe kwa njia ya Utume… Halafu eti katika wakati kama huu linazuka tangazo kama hili linalotoa sura mbaya kama si sura ya ovyo kabisa juu ya uhalisia wa Khilafah hasa kwa hao walio na uwezo mdogo wa kupima mambo (kisheria)…

Yote haya yanaleta kujiuliza swali bali maswali mengi sana…  Kwa kutangaza muda huu tangazo hili bila ya kuwepo mtawala wa wazi na hata hawa wenye kutangaza hawana uwezo wa kulinda amani ya ndani wala ya nje bali tu ni kwenye  mtandao wa kijamii wa facebook au vyombo vya habari… Hakika utangazaji wa muda huu unatia wasiwasi na hasa kwa kipindi hiki ambacho kumetapakaa vikundi vya kisilaha visivyojengwa kwa msingi thabiti wa kifikra. Hivyo kuwa ni rahisi kujipenyeza na kuingiza vibaraka waovu wa nchi za Mashariki na Magharibi ndani ya safu zake kwa usahali sana. Ni wazi kuwa nchi za Magharibi na Mashariki zinaufanyia vitimbi Uislamu na Khilafah na wanashughulika sana kuichafua Khilafah kwa kuwa wameshindwa kabisa kutajwa kwake. Basi makafiri wanakusudia kwa hadhari kubwa kwamba Khilafah ibakie kuwa ni tamko tu anajipachika atakayejisikia bila ya kuwa na vigezo, sifa wala uzito wowote. Basi jambo zito litakalowatia kiwewe makafiri ni vipi tena liwe jina kuwa ni la kawaida tu wanaloliimba maadui usiku kwa mchana…!

Enyi ndugu watukufu,

  1. Zaidi ya yote haya wafanyayo hawa waovu sisi tunawahakikishia maadui wa Uislamu wa Mashariki na Magharibi, vibaraka wao, wafuasi wao na majahili wao kuwa Khilafah ambayo iliongoza dunia kwa karne kadhaa ni yenye kufahamika na sio kwamba haifahamiki, na hila na vitimbi vyao vitaanguka patupu.

((وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللَّهُ وَاللَّهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ))

Wanafanya vitimbi na Allah ana vipindua vitimbi vyao na Allah ni mbora wa kupindua vitimbi﴿ (TMQ 8:30)

Kwa hakika Allah Mwenye Nguvu na Mshindi ameifungamanisha Khilafah na Hizb iliyo na wanaume wasio shughulishwa na biashara wala kuuza mbele ya utajo (dhikri) wa Allah wanaifahamu Khilafah ilivyo kwa nyoyo zao, masikio na macho yao na wakajiandaa kwa maandalizi ya ukweli na wakavua (istinbaat) hukmu zake na katiba yake kutokana na vyanzo vya Uislamu, ikiwemo muundo wake katika utawala na idara. Wanafanya kazi ya kuisimamisha Khilafah kwa kufuata vilivyo manhaj ya Mtume (saaw) bila kwenda kombo hata kidogo… Hakika wao, kwa idhini ya Allah, ni walinzi wa kweli wasiokubali uchafuzi wa aina yoyote na vilevile wao ni jabali kwalo juu yake, kwa usaidizi wa Allah, kutavunjika vitimbi na njama za makafiri na vibaraka pamoja na wafuasi wao. Na wao Hizb kwa msaada wa Allah ni wanasiasa weledi  ambao kwa nguvu za Allah watakabiliana na vitimbi vya maadui wa Uislamu na Waislamu. Vitimbi ambavyo vitawarejea kwao makafiri:

وَلَا يَحِيقُ الْمَكْرُ السَّيِّئُ إِلَّا بِأَهْلِهِ

Na vitimbi  viovu haviwazunguki ila waovu wake(waasisi) ﴿

(TQM 35:43)

Enyi ndugu watukufu,

Hakika suala la Khilafah ya Kiislamu ni jambo kubwa na adhimu, na kusimama kwake haitokuwa ni khabari zinazozungumzwa tu na vyombo vipotoshaji vya habari, bali itakuwa kwa idhini ya Allah, ni kishindo kikuu kitakachobadilisha misimamo ya kimataifa na itabadilisha sura ya historia na muelekeo wake… Hakika Khilafah itarudi kwa manhaji ya Utume kama alivyobashiri Mtume (saaw) na watakosimamisha watakuwa ni sawa na wale walioisimamisha Khilafah Rashida ya mwanzo. Wachamungu na wasafi wa matendo. Wao watau upenda Ummah, na ummah utawapenda, watawaombea dua Ummah, na ummah utawaombea, watafurahi kukutana na Ummah, na Umma utaona raha na utulivu kukutana nao, na wala hawaoni karaha kuwa nao pamoja… Na hivi ndivyo watakavyokuwa watu wa Khilafah ijayo kwa manhaj ya Utume. Allah atawapa Khilafah wenye kustahiki, na sisi tunamuomba Allah tuwe ni miongoni mwa hao wenye kustahiki na wahusika wake. Na tunamuomba
Subhana aturuzuku kuweza kuisimamisha.

فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُمْ بِهِ

Na furahini kwa baia yenu ambayo mumempa﴿

(TMQ 9:111)

Na wala musikate tamaa na Rehma za Allah. Kwani Allah hazipotezi juhudi mulizokwishazitoa, na wala hatozirudisha dua mulizokwisha ziomba kwake, na wala hatoyatupa chini matarajio yenu muliyoyatarajia . Kwa hivyo tusaidieni kwa kutoa juhudi zaidi na muonesheni Allah uchamungu wenu atakuzidishieni kheri na maneno ya mpuuzi yasikuvunjeni moyo kuacha kazi yenu iliyo na azma ya kweli.

Wassalamu Alaikum Wa RahmatuLlahi Wa Barakatuh.

3 Ramadhan 1435H     01/7/2014  Miladi

Mwisho wa majibu niliyotuma awali.

Namuomba Allah kwamba jibu hili litosheleze. Allah Akupeni mafanikio na msaada wake. Allah pia Atuongoze katika jambo la haki
Ndugu yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!