Kutumwa Kikosi cha Dhat As-Salasil

5

Katika mwezi kama huu wa Kiislamu tunaoendelea nao wa Jumada Ath-Thaniy, Mtume SAAW  alituma kikosi maalumu (sariya) kwa ajili ya kupambana na baadhi ya makabila ya mabedui wa kiarabu hususan Bani Quda’a katika maeneo ya mipaka ya Sham. Kimsingi hatua hiyo ya Mtume SAAW ililenga kukabiliana na kuuvunja nguvu ya utawala wa Kirumi (Byzantine). Utawala huo wakati ule ulikuwa ukilitawala kisiasa eneo lote la Sham. Eneo linalojumuisha ardhi yote ya leo ya Syria, Lebanon, Jordan, Palestina nk. Baadhi ya makabila ya mabedui yaliokuwa yakiishi mipakani na Sham yalikuwa washirika wakubwa na kuwa na ukuruba mkubwa na  dola ya Warumi (Byzantine) katika kutenda uadui dhidi ya Waislamu na dola yao.

Kikosi kilichotumwa na Mtume SAAW kinajulikana kwa jina la Dhat As- Salasil kilichotumwa ndani ya mwaka 8 Hijiri nchini ya uongozi wa Sahaba Amr bin Al-As  (Ra )

Mtume SAAW akiwa Amiri jeshi Mkuu wa dola ya Kiislamu alimkabidhi kamanda wa kikosi hicho Amr ibnul- Ass bendera maalumu ya Kiislamu katika msafara wake na kumpatia mujahidinna karibu 350 wakiwemo wapiganaji werevu. Aidha, Mtume SAAW alimtaka kamanda wake lau hali ya kivita itakuwa ngumu basi ayatake makabila ya maeneo hayo yaliyosilimu na ambayo yana mahusiano mazuri na Waislamu yasaidie katika mapigano hayo. Miongoni mwa makabila yaliokuwa kandokando na medani ya vita yalikuwa ni makabila ya Bali, Udhra na Balqa.  Kama kawaida Mtume SAAW alidhihirisha uerevu mkubwa wa kisiasa kwa kumteua Amr Ibn Al-Ass kuwa kamanda wa kikosi hicho, kwa kuwa pia nasaba ya ubabani kwake ilikuwa karibu na kabila la Bali.

Kwa kuwa jihadi ni ala au chombo cha kubebea siasa ya nje ya dola ya Kiislamu kwa kuondoa kila aina ya kizuizi kilichoko katika kuwafikishia wanadamu nuru, ukweli, uadilifu na usalama wa Uislamu na kuutawalisha Uislamu juu yao katika nyanja zote bila ya kuwalazimisha kusilimu, harakati za kijeshi za kikosi hiki cha Dhat As- Salasil dhidi ya Warumi na washirika wake hazikuwa za mwanzo wala za mwisho.

Kampeni dhidi ya dola ya Kirumi ilikuwa ni kampeni endelevu. Kwa mfano, mwezi mmoja tu kabla ya kutumwa kikosi hiki, Waislamu walipigana na Warumi katika Vita vya Mutah. Vita vilivyokuwa vikali dhidi ya dola ya Kirumi vikiongozwa na majemadari wakubwa wanne wa Kiislamu.  Wote wanne walikufa mashahid kishujaa na kwa ujasiri wa kupigiwa mfano. Na ukiangalia sababu msingi ya kutokea vita vya Mutah, ni baada ya Shurahabiil bin Amr Al-Ghassan, Gavana wa Warumi katika eneo la Al-Balqa na mshirika wa karibu wa Caesar, mtawala wa Kirumi, kumuuwa kwa dhulma sahaba Al-Harith Umair Al-Azdi, balozi  wa dola ya Kiislamu aliyetumwa na Mtume SAAW kufikisha barua ya ulinganizi wa Uislamu.

Kikosi cha Dhat As-Salasil kilikabiliana na jeshi kubwa la makafiri kiasi cha Mtume SAAW kuongeza nguvu kutoka Madina, makao makuu ya dola. Kikosi cha kutia nguvu kilikuwa chini ya sahaba Abu Ubaidah bin Al-Jarrah (Ra). Na vikosi vyengine vidogo vidogo vilitumwa zaidi ambavyo ndani yake walikuwemo masahaba wakubwa kama Umar na Abubakar (Ra). Waislamu licha ya uchache wa idadi  yao na zana walifanikiwa kupenya ndani ya ngome ya kabila Qudaa, wakapigana kishujaa na kwa ujasiri  mpaka wakapata ushindi.

Huo haukuwa mwisho wa Waislamu kukabiliana na Warumi. Kwa kuwa jihadi ni ibada inayoendelea kama ibada nyengine, bali mwaka uliofuata Mtume SAAW aliandaa  jeshi, na yeye  binafsi kushiriki   katika vita vikali sana vya Tabuk dhidi ya hao hao Warumi mipakani mwa Syria. Pia Siku chache kabla ya kufariki kwake SAAW, alituma kikosi cha kupambana na hawa hawa Warumi chini ya uongozi wa  Kamanda kijana, Usamah bin Zaid.

Mapambano hayo yaliendelea hata baada ya kufariki  Mtume SAAW katika zama za makhalifa akiwemo  kama Vita vya Yarmouk nk.

Hatimae ndani ya mwaka 1453 chini ya Khalifah Muhammad Al-Fatih, makao makuu ya dola ya Kirumi  ndani ya  mji wa Constantinople/Istanbul, Uturuki ya leo ukafunguliwa rasmi (fathi) na kuwa chini ya himaya ya Waislamu na dola yao.  Tukio hilo kubwa na tukufu lilikuwa ni bishara iliyoajwa na Mbora wa viumbe na Mkweli wa kauli,  Mtume  wetu SAAW  kwa kauli yake :

“Mtaufungua (fathi) mji wa Cosntantinople. Amiri wake atakuwa Amiri bora, na jeshi lake litakuwa jeshi bora”.

(Ahmad na Al-Hakim)

Afisi ya Habari –  Hizb ut- Tahrir Tanzania

24 Jumada al-thani 1439 Hijri   | 12-03-2018 Miladi

https://hizb.or.tz/

https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania

5 Comments
 1. Vcrsad says

  buy generic levofloxacin 500mg order levofloxacin 250mg without prescription

 2. Liawhp says

  buy avodart 0.5mg sale flomax 0.4mg us purchase zofran sale

 3. Rubygv says

  spironolactone order fluconazole 200mg without prescription cost fluconazole 200mg

 4. Espypr says

  ampicillin uk ampicillin 250mg drug buy erythromycin 250mg pills

 5. Onqdft says

  order fildena 100mg online cheap brand nolvadex robaxin 500mg tablet

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.