Kuuza Tunda Lililo Kwenye Mti

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

Swali:

Mwanachuoni wetu kipenzi na Amiri, Assalamu Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh. Nchini kwetu kuna kitendo cha kuuza mazao wakati yapo kwenye mti kabla ya mavuno. Kwa mfano mazao kama karafuu, pilipili, nazi n.k  yanauzwa namna hiyo. Mwenye shamba hupanda, kumwagilia maji, hutia mbolea ili kuongeza zaidi mazao na matunda yakizaliwa kwenye mti, matunda hayo huuzwa kwa bei ya makisio, kwahiyo, mnunuzi inambidi avune na ayashughulikie ipasavyo. Mnunuzi atamlipa muuzaji (mwenye shamba) bei waliyokubaliana kabla ya mavuno. Mara tu mauzo yakifanyika(bei wanakubaliana muuzaji na mnunuzi) yule muuzaji (mwenye shamba) anakuwa hana dhamana tena ya mazao, na yule mnunuzi anaweza kuyavuna kwa haraka au anaweza akayachelewesha mpaka akiona sasa tayari, lakini ni jukumu lake kuyalinda yale mazao kutokana na wanyama, wezi n.k. Je jambo hili linaruhusiwa katika Uislamu? Allah akupe baraka na aupe ushindi ummah huu chini ya uongozi wako. Mwisho.

Jawabu:

Waalaykum Salam Warahmatullah Wabarakatuh,

Swali lako nimefahamu kwamba unauliza kuhusu kuuza tunda lililo kwenye mti, yaani mtu anakwenda kwa mwenye mti na kumwambia nataka kununua tunda la mti wa tini  huu kwa msimu wote na yanakuwa matunda ya mti ni yangu, na nakula na kuuza mpaka matunda ya mti yamalizike msimu huu. Na wanawafikiana juu ya hayo kwa malipo maalum… Na wewe unauliza ikiwa jambo hili linafaa.

Ikiwa hivyo ndivyo basi jawabu lako ni hili:

Naam, muamala huu umeenea katika nchi za Waislamu na katika fiqhi unaitwa “kuuza matunda hali ya kuwa bado yapo kwenye asili yake” (Bai’u thimaar wahiya ‘ala usuulihaa), na huitwa na wengi “Dhamana ya mti” (Dhwamanu shajar)… Hii inafaa (jaaiz) lakini kwa sharti yawe yale matunda yameshadhihiri uzuri wake  na si lazima kuwa yameiva yote kwani hayaivi yote kwa pamoja kwa wakati mmoja. Na kunukulia hapa baadhi yalioyoelezwa na dalili kwa kina kutoka kitabu chetu cha Shakhsiyyah ya Pili mlango wa “Kuuza matunda hali ya kuwa bado yapo kwenye asili yake”:

(Na hukmu ya kisharia katika dhamana hii yaani katika kununua matunda yaliyopo juu ya mti yaani bado yapo kwenye mti wake ina ufafanuzi. Hayo ni kwasababu yanaangaliwa yale matunda, ikiwa umedhihiri uzuri wake, yaani yamefikia uwezekano wa kuyala basi inafaa dhamana (dhwamaan) hii, yaani inafaa kuyauza matunda katika hali hii. Lakini ikiwa bado matunda hayajadhihirisha uzuri wake, yaani ikiwa hayajaanza kufikia kuliwa, hapo itakuwa haifai kuyauza. Na hayo ni kwa yale aliyopokea Muslim kutoka kwa Jabir (RA) amesema: «نهى رسول الله عن بيع الثمر حتى يطيب»

“Mtume (SAW) amekataza kuuza matunda mpaka yawe mazuri”.

Na kwa yale yaliyopokelewa kutoka kwake vilevile kwamba amesema: «نهى رسول الله … وعن بيع الثمر حتى يبدو صلاحه»

“Mjumbe wa Allah (SAW) amekataza …na kuuza matunda mpaka udhihiri uzuri wake”. Na kwa yale aliyoyapokea kwake Bukhar vilevile kwamba amesema: «نهى النبي عن أن تباع الثمرة حتى تشقح، قيل ما تشقح، قال: تحمار وتصفار ويؤكل منها»

“Mtume amekataza kuuzwa matunda mpaka ya-tashaffah, pakasemwa nini tashaffah, akasema: yapige wekundu na yapige umanjano na yaliwe (yaweze kuliwa)”. Na kwa yale aliyoyapokea Bukhar kutoka kwa Anas ibn Malik kutoka kwa Mtume : «أنه نهى عن بيع الثمرة حتى يبدو صلاحها، وعن النخل حتى يزهو، قيل: وما يزهو؟ قال: يحمار أو يصفار»،

“Kwamba hakika yake amekataza kuuza matunda mpaka udhihiri uzuri wake na mtende (tende) mpaka i-yazhuu, pakasemwa nini yazhuu? Akasema: Ipige wekundu au ipige umanjano”

Na kwa yale yaliyopokelewa kutoka kwake pia:«إن رسول الله نهى عن بيع الثمار حتى تُزْهي، فقيل له: وما تُزْهي؟ قال: حتى تحمر. فقال رسول الله : أرأيت إذا منع الله الثمرة بم يأخذ أحدكم مال أخيه»

“Hakika ya Mjumbe wa Allah amekataza kuuza matunda mpaka ya-tuzhii, pakasemwa kuambiwa yeye: Nini tuzhii? Akasema: Mpaka yapige wekundu. Mjumbe wa Allah akasema: Waonaje Allah akizuia matunda je kwa kitu gani mmoja wenu atapata mali ya ndugu yake”.

Na kwa yale yaliyopokelewa na Bukhar kutoka kwa Abdillah ibn Umar kwamba Mjumbe wa Allah:

«نهى عن بيع الثمار حتى يبدو صلاحها، نهى البائع والمبتاع»“Amekataza kuuza matunda mpaka udhihiri uzuri wake, amemkataza muuzaji na mnunuzi”.

Na katika riwaya ya Muslim kwa lafudhi: «نهى عن بيع النخل حتى يزهو، وعن السنبل حتى يبيض ويأمن العاهة»“Amekataza kuuza mtende (tende) mpaka ipige wekundu au ipige umanjano, na sunbula (aina ya mti – ambary – hutumika pia kufanyiwa mafuta) mpaka iwe nyeupe na iwe haina maradhi”.

Hadithi hizi zote ziko wazi katika kukataza kuuza matunda kabla ya kuiva. Basi hutumia kwa dalili kinachotajwa (mantuuq) katika hadithi hizi kuhusu kutofaa (‘adam jawaaz) kuuza matunda kabla ya kudhihiri uzuri wake. Na hutolewa dalili ya ufahamu wake (mafhuum) kuhusu kufaa (jawaaz) kuuza matunda utakapodhihiri uzuri. Na kwahiyo, hakika dhamana ya mti (dhwamaanu shajar) ambao umedhihiri matunda yake kama vile zaituni (olive), malimau, tende na yasiyokuwa hayo,  inafaa ukidhihiri uwezekano wa kuliwa. Na haifai ikiwa haujadhihiri uwezekano wa kuliwa.

Na kule kudhihiri uzuri katika matunda ni (uwezekano wa) kuliwa kwake, ndicho kinachofahamika katika hadithi zilizopokelewa kuhusu hilo. Na hakika kuziangalia kwa kina hadithi zilizopokelewa katika kukataza kuuza matunda kabla ya kudhihiri uzuri wake, tunakuta kwamba hadithi hizo zimepokewa tafsiri kadhaa kuhusu hadithi hizo. Katika hadithi ya Jabir imepokewa: «حتى يبدو صلاحه» “Mpaka udhihiri uzuri wake”. Na imepokewa: «حتى يطيب» “Mpaka iwe nzuri”, na katika hadithi ya Aniis:«نهى عن بيع العنب حتى يسودّ، وعن بيع الحب حتى يشتد» “Amekataza kuuza zabibu mpaka iwe nyeusi, na kuuza nafaka mpaka ipee”. Imepokewa na Abu Daud.  Na katika hadithi nyengine ya Jabir: «حتى تشقح» “Mpaka udhiri wekundu au umanjano”. Na katika hadithi ya Ibn Abass: «حتى يطعم»“Mpaka yalike”, kwahiyo, hakika hadithi zote hizi zimekusanya maana moja nayo ni ‘mpaka yaanze kulika’. Na kwa kuangalia hali halisi ya matunda huonekanwa kwamba mwanzo wa kulika hutofautiana kutokana na tofauti ya matunda.

Kati yao yapo yanayoanza kulika kwa kubadilika rangi yake mbadiliko wa dhahiri, hicho kinachodhihirika hujulisha kuiva, kama vile tende (albalh – aina ya tende), tini, zabibu, pea, na mfano wa hayo. Na kati yapo yanayodhihiri uivaji kwa kubadilika au kwa kuliangalia kwa wale wajuzi kama tikitiki maji kwasababu ya ugumu wa kufahamu mbadiliko wa rangi yake kwa kuiva. Na yapo yanayodhihiri ulaji wake kwa kule kuanza kubadilika maua kuwa matunda kama matango, qithaa (aina ya matango huwa marefu), na mfano wa hayo. Kwahivyo, kinachokusudiwa kudhihirika kwa uzuri katika kila tunda ni kudhihiri uzuri wake kwa ajili ya kuliwa. Na dalili ya hilo kile alichopokea Muslim  kutoka kwa Ibn Abass kwamba amesema: «نهى رسول الله عن بيع النخل حتى يأكل منه أو يؤكل»“Mjumbe wa Allah amekataza kuuza tende mpaka iliwe au iwe tayari kuliwa” . Kama inavyotoa dalili hadithi ambayo Mutafaqun ‘alayhi  katika riwaya ya Jabir: «حتى يطيب»“Mpaka liwe zuri”. Na kwa haya hubainika kufaa kuuza tunda la qithaa, tango, na mfano wake, yaani kufaa dhamana ya mtango kwa kule kuanza kutoa matunda yake tu, yaani kwa kule kuanza tu kubadilika maua kuwa matango na kuenea yale matango nayo ni maua na kabla ya kutawanyika maua yaani kuenea yale matunda (matango) katika hali hii kabla ya kupatikanwa, kwa mujarad wa kupatikana chochote tu katika hayo matunda (matango).

Na haya si katika mlango wa kuuza kisichokuwepo (alma’aduum), kwasababu matunda yake yanazaliwa kwa kufuatana hayapatikani mara moja (yote kwa pamoja). Basi huuzwa matunda ya mtango yote kwa msimu wake wote yaliyopo (yaliyokuwa tayari yameshazaliwa) na yaliyokuwa hayapo bado (bado kuwa tayari kuzaliwa). Kwasababu hakuna tofauti kati ya kudhihiri uzuri wa tunda kwa kupiga wekundu kama tende au kwa kupiga weusi kama zabibu au kwa kubadilika rangi kama pea na baina ya kudhihiri uzuri wake kwa kudhihiri baadhi yake na maua kufuatana baadhi yao kutoa matunda yake. Isipokuwa tunda ambalo hauzingatiwi mwanzo wa kubadilika maua yake kuwa matunda kama tikiti maji haifai hayo kwalo, kwahiyo, haifai kuuza lozi hali ya kuwa ni ua, wala kuuza tini hali ya kuwa ni bado ngumu kabla haijaanza kuiva. Na kusudio la kuyauza matunda hali ya kuwa yapo juu ya mti, yaani ni dhamana ya mti, kwasababu kuuza matunda bado yapo juu ya mti kumefungika (muqayyad) na kudhihiri uzuri wake, yaani kudhihiri kinachomaanisha kuanza kuiva (kupea) kwa matunda.

Na si kusudio la kudhihiri uzuri wa tunda kudhihiri uzuri wa matunda yote, hakika hili ni muhali, kwasababu matunda huiva moja moja au kadhaa hivi kisha tena hufuatana mfululizo. Na si kusudio kudhihiri uzuri bustani yote kwa wakati mmoja wala kudhihiri uzuri bustani yote, bali kusudio la kudhihiri uzuri wake ni kudhihiri uzuri wa tunda husika ikiwa hazitofautiani aina zake kiuivaji kama zaituni (olive), au kudhihiri uzuri wa aina (type) yake ikiwa aina zake zinatofautiana kiuivaji kama tini na zabibu. Kwamfano, ukidhihiri uzuri wa baadhi ya matunda ya mtende katika bustani itafaa kuuza matunda ya mtende yote katika bustani yote. Na ukidhihiri uzuri wa aina ya matofaa (peasi) katika baadhi ya miti (mitofaa), itafaa kuuza aina hiyo ya matofaa (peasi) katika bustani yote. Na ukidhihiri uzuri wa zaituni katika miti kwenye bustani basi inafaa dhamana ya zaituni katika bustani yote.

Kwasababu hadithi inasema:«نهى عن بيع النخل حتى يزهو وعن السنبل حتى يبيض ويأمن العاهة» “Amekataza kuuza mtende (tende) mpaka ipige wekundu au ipige umanjano, na sunbula (aina ya mti – ambary – hutumika pia kufanyiwa mafuta) mpaka iwe nyeupe na iwe haina maradhi”.

Na anasema:«نهى عن بيع العنب حتى يسود، وعن بيع الحب حتى يشتد» “Amekataza kuuza zabibu mpaka iwe nyeusi, na kuuza nafaka mpaka ipee”, kwahiyo, imebainisha hukmu ya jinsi ya matunda yote  yenyewe hasa na kila aina yenyewe hasa , akasema katika nafaka mpaka ipee, na katika zabibu nyeusi mpaka ipige weusi. Kwahiyo, hukmu imeshikana na kudhihiri uzuri wa jinsia zote (za matunda) bila kuangalia jinsia zilizobaki (ambazo hazijatajwa), na kila aina bila ya kuangalia aina nyengine (zilizokuwa hazijatajwa). Na neno kudhihiri uzuri lililopokelewa katika hadithi kuhusu jinsi moja na kuhusu aina moja, husadikisha katika baadhi ya matunda hata yakiwa kidogo kiasi gani, zaidi ni kwamba hali halisi ya matunda inaonesha kwamba yanafuatana (kupevuka na kuiva).

Na kwa hayo, inabainika kwamba inafaa dhamana ya mti wowote, yaani kuuza tunda la mti wowote kabla ya kudhihiri uzuri wake…

Nataraji jawabu litakuwa limekaa wazi.

Ndugu yenu Atta Ibn Khalil Abu Rashtah

17, Jamad Al-ula 1438H

14/02/2017

Maoni hayajaruhusiwa.