Matokeo ya Ulinganizi Sio Jukumu la Mlinganiaji

Ubebaji wa da’wa ni kazi ya Mitume, ni kazi bora na yenye heshima sana. Allah (SWT) amesema:

“Na ninani mwenye kauli bora kuliko yule aitae watu kwa  Allah, na mwenye kufanya vitendo vizuri, na kusema kwa matendo na maneno kwamba mimi ni miongoni mwa waislamu?” (41:33),

Malipo ya kazi hiyo, zawadi bora na kubwa mno, Wale wote wafanyao kazi hiyo ya heshima watapata pepo ya daraja ya juu na sehemu bora kabisa huko akhera. Hili lawezekana ikiwa watafanya kazi hiyo kwa ubora, kwa kukamilisha kazi yao  na kuifanya kwa ajili ya Allah (SWT).

Ili mbebaji da’wa awe makini na da’wa yake, aweze kujiamini na asiyumbishwe na mazonge , wala kuvurugwa kiasi ambacho akaachana na da’wa yake, lazima ashikamane na vitendo na njia yake kutoka katika kitabu cha mola wake na sunnah za Mtume wake. Hili litamfanya awe makini na jambo lake kama Allah asemavyo:

“Sema, hii ndio njia yangu, ninalingania kwa Allah kwa ujuzi, mimi nafanya hivi na kila wanaonifuata, wala mimi sio miongoni mwa wanaomshirikisha Allah”. (12:108).

Jambo linalotakiwa kuwekwa wazi, ukweli unaotakiwa kufahamishwa na kuwekwa sawa ni jukumu na asili ya ubebaji da’wa. Ni kujitwika jukumu la ufikishaji pekee, na je jambo hilo linaishia hapo tu..? Au mbeba da’wa anawajibika na matokeo ya da’wa yake na awajibishwe kwa hilo ?

Kujibu hilo swali , ni muhimu kueleza yafuatayo:

1 ) kuna makumi ya aya katika Qur’an yanayothibitishi utofauti na utengano kati ya jukumu la ufikishaji na matokeo ya ufikishaji da’wa, hata ingawa mbebaji hutaraji mafanikio ya da’wa yake na kufata kwake maelekezo kwa watu wake. Hizi ni baadhi ya aya hizo:

“Na mkikengeuka basi jueni juu ya Mtume wetu ni kufikisha tu ujumbe wazi wazi (Al-Balaagh al Mubeen)” (5:92).

“Jukumu la Mtume ni kufikisha ujumbe kwa usahihi.” (24:54).

“Na wakikupuuza na sisi hatutakupeleka uwe ni mwenye kuwalinda, si juu yako ila kufikikisha tu).” (42:48).

Aya zaonyesha kwamba jambo la ufikishaji da’wa ni lingine na kukubaliwa jambo hilo lipo katka uwezo wa Allah (SWT); mbebaji da’wa hana uwezo nalo hilo: Hizi ni katika aya hizo:

“Sio kwako bali ni maamuzi ya Allah, ikiwa atawahurumia au atawaadhibu, kwa kule kufanya kwao maovu ,” ( ),

“Hivyo tunakukumbusha kwamba wewe ni mkumbushaji. Hauna zaidI ya hilo kwa mambo yao.” (88-21/22).

2 ) kushikana na imani na matendo mema, inaashiriwa na maneno ya Allah (SWT);

“Allah amewaahidi, kwa wale wanao amini miongoni mwenu  na kufanya vitendo vizuri kwamba atawapa ukhalifah katika ardhi.” (24:55).

Hili sio lazima likupelekee katika kupata khilafah au ushindi, ushahidi wa hilo ni huu ufuatao:

a) Kuchelewa kwa ushindi wa Mitume, ikiwa Masahaba pamoja na Mtume wetu Muhammad (SAW), ingawa walikua wamejidhibiti katika imani na matendo mema tena bila shaka ya hilo. Allah (SWT) amesema :

“Hata Mitume walipokata tamaa, na makafiri wakadhania wameambiwa maneno ya uongo. Hapo ndipo msaada wetu ulipowajia” (12:110) .

“Na mnadhani mtaingia pepeni, na hamjapatwa na yaliowapata kabla yenu? walipatwa na mashaka na madhara na wakatetemeshwa sana, hata  Mtume na walio pamoja nao wakasema, itakuja lini nusra ya Allah, na kwah akika nusra ya Allah ipo karibu!” (2:214).

b) Muhimu kwa mbeba da’wa kuwa na uvumilivu na subra hadi pale  Allah (SWT) atakapotekeleza ahadi yake na kumlipa malipo bora. katika hili, Allah (SWT) anasema:

“Mtapata misukosuko katika mali zenu na nafsi zenu ,na mtasikia udhia mwingi kwa wale waliopewa kitabu kabla yenu ,na kwa wale walioshirikisha. Na kama mkisubiri na kujilinda kwa yale aliokataza Allah mtakuwa mmefanya jambo zuri, kwani mambo haya ni katika makubwa katika kuazimia mtu kuyafanya…. “ (3:186).

“Na walikadhibishwa Mitume kabla yako, wakavumilia kwa kule kukadhibishwa na kudharauliwa hadi ikawafikia nusra yetu, na hakuna abadilishae maneno ya Allah” (6:34).

c) Onyo kali dhidi ya hisia za kutokua na subra, hasira, kutokuhisi maumivu ya watu na ujeuri. Nyingi katika aya na hadithi zimeonya katika hayo Allah SWT anasema:

“Basi subiri kwa hukmu ya Mola wako, wala usiwe kama mmezwa na chewa … “ (68:48)

Agizo la Allah katika sehemu ifuatayo, ambayo anatoa muda kwa makuraishi na kuchelewa msaada kwa Mtume wa Allah dhidi yao. “Pia kama Allah angetaka angewakusanya katika dini ya sawa. Hivyo usiwe kama hao wajinga .” (6:35) Na akaseama  (SWT):

“Je yule aliepambiwa amali zake mbaya akaziona ni nzuri, utamwambia nini hata asikie ? Bila shaka mwenyezi mungu humuacha kupotea amtakae na humuongoa amtakae. Hivyo basi roho yako isitoke kwa majonzi juu yao, kwayakini  Allah anajua wayafanyayo.” (35:8). Mtume  (SAW) amesema wakati akizungumza na Khabab bin al Aratt mwisho mwa hadithi:  “. . . .usiwe na unapupa.”

3) Ni muhimu mno kwa mbeba da’wa kufahamu uzito wa majukumu yake. Majukumu ya uhuishaji na mabadiliko na anapaswa kufahamu ukubwa wa changamoto, vikwazo na majaribu atayapata kwa kubeba kwake da’wa. Hii ni sehemu muhimu sana katika kupima sana kwa mbeba da’wa.

Haipingiki kwamba wabeba da’wa wa leo ambao wamejifunga katika da’wa ya haki na man-haji sahihi wamepitia magumu tangu zamani hadi sasa. Na hii ni sawa kabisa na alivyoesema Mtume Muhammad (saw):

“Uislamu ulianza kama kitu kigeni, na utakuja kuonekana kama kitu kigeni, furaha na malipo ni kwa wale watakao onekana ni wageni.”

Mbali na hivyo, tangu wabeba da’wa walipoanza mchakato wa kimabadiliko, na urudishaji maisha ya kiislamu, walikutana na changamoto ya namna gani ya urejeshaji na njia ya kimabadiliko pindi walipoamiliana na wale waliotoka katika njia ya Mtume (saw) katika usimamishaji wa dola ya kiislamu na utabikishaji wa sheria za Allah katika ardhi. Zaidi ya hayo, hali ya kiulimwengu hivi sasa ni tofauti na zama za Mtume Muhammad (saw) alipotabikisha dola yake. Dola ilitabikishwa madina bila tafrani kutoka uajemi wala rumi. Makutano ya kwanza ya mapigano kati ya dola ya kiislamu na kiroma yalitokea mwaka wa 8 baada ya Hijra. Leo hii, dola za kikafiri katika dunia zinafanyakazi kwa pamoja kuzuia urejeshwaji wa dola ya kiislamu ya khilafah . Pia wanapambana na siasa ya kiislamu baada ya kufanikiwa kuangusha khilafah miaka zaidi ya 70 iliyopita.

Changamoto ambazo wabeba dawa wanazipitia kwa ujumla hivi sasa ni nyingi na hizi ni miongoni mwake.

a). Changamoto za kimaumbile: Hizi huangazia zaidi kuharibiwa kwa khilafah, kuanzishwa kwa umbile la kiyahudi katika Palestina, kuwawinda wanaofanya kazi za kurejesha uislamu kwa kutumia mbinu za kikatili tofauti na zilizopita, kuuzuia ummah kupata uwezo wa kuwa zana za kisasa za upiganiaji kama silaha za Nyuklia na silaha za kikemikali na kuua na kushambulia yoyote anaejaribu kuunganisha ummah.

b). Changamoto za kisomi: Hizi huletwa katika kupaka matope taswira ya uislamu na kuwavuruga waislamu popote walipo, haswa kupitia wasomi wa hovyo hovyo. Pia kutumia mbinu za utaifa na urangi, kupitia fikra za ukombozi na demokrasia. Zaidi, wanaleta ufahamu wa kulenga zaidi kuharibu mfumo wa kijamii wa kiislamu na kudai hauwezi kutatua changamoto za sasa na nyinginezo.

Uwepo wa changamoto na vikwazo hivyo ambavyo wabeba da’wa wa hivi sasa wanavipata, mbali na jukumu zito walilonalo ni mambo ya kawaida na kimaumbile hutokea haswa katika ubebaji wa da’wa. Pamoja na hayo hairuhusiwi kwa mbeba da’wa kuyumbishwa au kuacha da’wa pindi anapohisi vikwazo na kuchelewa kwa ushindi. Anapswa kufahamu kwamba kutojibiwa na jamii na watu kutounga mkono da’wa na kuchelewesha ushindi, yote hayo hayamaanishi ni matokeo ya kukosea kwake njia. Hii sio dalili ya sawa ukilinganisha na ile hali ya ubebaji da’wa katika mji wa Makkah. Yanayobakia yapo katika uwezo wa Allah (Swt). Ibn Hisham amenukuliwa katika sira yake ya Mtume (SAW) , “Na pindi Allah SWT alipotaka kuisaidia dini yake, kumsaidia Mtume wake  na kutekeleza ahadi kwake, Mtume wa  Allah (SAW) alikua akienda nje kwa nyakati fulani akikutana na watu wachache katika answaar.”

Upendeleo huu kutoka Allah (SWT) juu ya Mtume wake ulikuja baada ya jamii ya Makka kuukataa ujumbe wake na Mtume wake, na baada ya makabila ya kiarabu kukataa kumpa nusra. Hivyo hali ilikua mbaya kupita maelezo.

Hivyo, baada ya maelezo hayo yaliyotangulia, mbeba da’wa afahamu kwamba yupo katika njia sahihi bila kujali itachukua muda gani kufika lengo. Pia atakiwa kuwa na matumaini na Allah (SWT) kwamba ushindi utakuja hivi karibuni hivyo asilinganishe ubebaji Da’awa na matokeo anayoyapata.

kuna jambo lingine, kitu ambacho mbeba da’wa atakiwa kuhakikisha muda wote ni kwamba vitendo vyake vinapaswa kuwa sahihi ili kufikia hilo vinapaswa kuwa vizur na safi. Vitendo vizuri ni vile vinavyoegemea katika sharia na sio kinyume chake. Vitendo safi vile vinavyofanywa kwa ajili ya Allah (SWT), na sio kwa ajili ya kupata kitu. Pindi ikiwa hivyo, basi mbeba dawa anapaswa kujihakikishia ahadi ya Allah itakua ni yenye kutekelezeka, na hivyo dola ya kiislamu itasimama, Hata kama itachukua muda.

Maoni hayajaruhusiwa.