Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania

0

Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania:

Ni mpango wa kibiashara ya dhulma na si vyenginevyo

Habari:

Vyombo vya habari  Tanzania vimeripoti juu ya hali ya kuchanganyikiwa na kuvunjika moyo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa kukosa mikopo ya elimu ya juu. Imethibitishwa kuwa wanafunzi wawili kati ya kila watatu walioomba wamekosa mkopo kwa mwaka wa masomo 2016-17. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imedai kuwa hali hii ni matokeo ya kuongezeka idadi ya vyuo vikuu na vyuo vya kati (colleges) jambo ambalo ni gumu kukabiliana nalo.

Maoni:

Serikali za kibepari zinawaaminisha watu kuwa kugharamia elimu kuwa ni jukumu na wajibu kwa mzazi au mlezi na sio jukumu la serikali. Kwa hivyo, anaebahatika kupewa mkopo huwa amefanyiwa ihsani na sio haki yake.

Mlolongo wa miaka mitano katika mchakato wa utoaji mikopo unadhihirisha wazi wazi kwamba hali ni mbaya ikielekea katika uoza zaidi. Takwimu zinaonesha kama ifuatavyo:

  • Mwaka 2012-13 wanafunzi walioomba mkopo walikuwa 45,651 waliobahatika kupewa ni 28,906
  • Mwaka 2013-14 waombaji walikuwa 53,650 na waliopewa walikuwa 33,316
  • Mwaka 2014-15 kulikuwa na maombi ya mkopo 60,085 na waliokubaliwa ni 29,731
  • Mwaka 2015-16 walipewa mkopo wanafunzi 54,072 kati ya maombi 70,718 na
  • Mwaka 2016-17 wanafunzi waliopewa ni 28,354 kati ya maombaji 83,225.S

Kwa uhakika, mikopo ya elimu ya juu kutoka serikalini haipo kumsaidia wala kuwapunguzia mzigo wanafunzi, wazazi au walezi, bali ni mpango wa kibiashara. Ndio maana Bodi ya Mikopo ina sera nyuma ya pazia ya kuchelewa kwa makusudi kufuatilia marejesho kutoka kwa wahitimu mara wakiajiriwa, hiyo ikiwa ni mbinu ya kuongeza mzigo wa riba wakati wa kulipa. Pia hatua yake iliyokosa ubinadamu ya karibuni ya kuongeza kiwango cha makato ya malipo ya marejesho kutoka 8% mpaka 15% kwa mrejesho wa kila mwezi inadhihirisha dhamira yao ya kibiashara na sio msaada. Makato hayo yatatia ugumu juu ya ugumu katika maisha ya waajiriwa wapya.

Wanafunzi, wazazi na walezi wanakabiliwa na hali ngumu katika upande wa elimu ya juu, sambamba na hilo Tanzania inapita katika kipindi kizito kiuchumi kwa kugubikwa na wimbi la mfumko wa bei.

Uislamu chini a Khilafah itatoa elimu bure kuanzia  chekechea hadi elimu ya kati, na  inatoa elimu ya juu  kama ya vyuo vikuu bure, kwa mujibu wa uweza wake. Kamwe haitoifanya elimu kuwa ni mpango wa kibiashara. Katika Uislamu elimu ni mali ya Ummah, na dola ya Khilafah ina dhamana kuhakikisha kila mtu anaipata kwa usahali.

Imeandikwa na Ali Amour

Mjumbe wa Afisi ya Habari- Hizb ut Tahrir Tanzania

Kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.