Mivutano inayoendelea baina ya Marekani na Korea Kaskazini

0

بسم الله الرحمن الرحيم

SWALI:
Mvutano unazidi kuwa mkubwa baina ya Marekani na Korea ya Kaskazini, na Marekani inafanya mazoezi makubwa ya kivita katika Korea ya kusini, wakati ukijiri mvutano huu Marekani imetuma kundi la meli kubwa za kivita ikiwemo ya kubebea ndege, wakati ambapo Korea ya Kaskazini imeonya kuzuka kwa vita vya nuklia. BBC ilisema tarehe 15/04/2017 ya kwamba (Korea ya Kaskazini imeionya Marekani kutokana na kitendo chochote cha kiuchokozi katika eneo. Inasema kwamba “ Iko tayari kujibu mashambulizi ya kinyuklia”.
Nini hakika ya mvutano huu? Je yawezekana kukazuka vita vya kinyuklia baina yao? Na upi msimamo wa China hali ya kuwa mvutano upo chini ya mipaka yake na hasa ikizingatiwa kuwa Korea ya Kaskazini ni mwenziwe?

JAWABU:
Ndio, mvutano umeongzeka kwa kiwango kikubwa baina ya Korea ya Kaskazini na Marekani baada ya rais Trump kuchukua nafasi ya uongozi Marekani. Na qadhia ya Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora yake, kwa Marekani anaitumia kuwa sababu ya kuitisha Korea ya Kaskazini. Na ilidhihirika kuongezeka kwa mvutano kwa kasi kubwa baada ya kutawala uongozi wa Trump Marekani. Kana kwamba uongozi huo umeingia na kipaumbele chake kikubwa ni kumaliza kile inachokiita “kitisho” cha Korea ya Kaskazini kwa maslahi yake na waitifaki wake katika Asia. Na katika yanaoyoashiria hayo ni:
1. Suala la Korea ya Kaskazini katika mkakati wa Marekani sio kuwa ni suala la nguvu za kijeshi za kiuadui. (Korea ya Kaskazini) ina nidhamu yake ya kijamaa na wala hainyenyekei nidhamu ya kilimwengu ya Kimarekani tu, kwani Korea ya Kaskazini ni ndogo na nguvu zake vilevile Marekani haiziweki kuwa kipaumbele kikubwa cha Marekani isipokuwa kuwa ni sehemu ya jumla ya ile inayoiwa China. Marekani inaangalia kwa hadhari kubwa maendeleo ya ukuaji wa China. Na inadurusu namna kadhaa za uwezekano wa kupunguza nguvu za China. Na katika mambo ya kuyafanyia kazi kadhaa ni kutengeneza hali ya mvutano kwenye mipaka ya China, miongon mwao ni Korea ya Kaskazini
Na linalothibitisha hayo ni kuwa Marekani katika kipindi cha Obama ilichangamka kujenga waitifaki karibu na China. Mahusiano yake na India, Japan, Vietnam na Ufilipino yakawa yanazidi waziwazi na pia Korea ya Kusini. Na ilitaka kutoka itifaki hii kuwa ni ngao ya kuizunguka China ili kuizuia siasa ya China ya kuekeza katika bahari ya kusini ya China na (kuzuia) kuziimarisha njia kuu za biashara zake na ulimwengu. Kawahiyo ikawa Marekani kuunda mazingira ya mvutano na Korea ya Kaskazini ni moja kati ya mivutano mengine ambayo Marekani imeiibua dhidi ya China. Kwa mfano, mzozo wa mpaka baina ya China na India. Na masuala ya visiwa baina ya China kwa upande mmoja na Japan, Ufilipino, Vietnam na Malaysia upande wa pili.

Na kwa sababu ya China, Marekani imeondoa vizingiti vingi vya kijesshi la Japani ili ipate kuikabili China.  Na leo Marekani inapoliweka suala hili la “kitisho” katika kipaumbele chake kikuu, hilo huwa ni katika sehemu ya mkakati wake dhidi ya China… Hakika shinikizo la Marekani dhidi ya Korea ya Kaskazini si jambo jipya hata ikiwa hivi sasa likiwa kali zaidi… Mkakati huu ulianza kwa mbinu ya shinikizo la mazungumzo. Basi mazungumzo ya Marekani na Korea ya Kusini yalitoa matunda ya mwaka 1994 ya kusimamishwa mpango wa nyuklia wa Pyong Yang.
Mwaka 2008 mazungumzo ya pande sita yalizaa matunda ya kufungwa kwa mtambo(reactor) wa Yongbyon. Na mwaka 2012 yalizaa matunda ya Korea Kaskazini kusitisha mpango wake wa nyuklia na kuruhusiwa kuingia kwa wakaguzi. Na kila mara Korea ya Kaskazini ilikuwa inarejea tena kuhuisha mpango wake wa nyukilia kwasababu ya Marekani kutotekeleza ahadi zake za kuipa mitambo (reactors) yake maji mepesi(light water)au kuipa nishati kama badili. Au kuidhalilisha kwa misaada inayoipa. Kwa hiyo Marekani ndio iliyokuwa inairejesha Pyong Yang kwenye mzunguko wa mvutano… Kisha Marekani katika mwaka 2012 ikashika mbinu mpya ambayo ni kusafirisha 60% ya jeshi lake la baharini kwenda mashariki ya mbali(far east). Na inafanya hayo si kwasababu ya Korea ya Kaskazini ambayo ni ndogo, lakini ni kwasababu ya kupunguza nguvu za China. Na mvutano unaotokea leo si chengine isipokuwa ni kukamilisha kupunguz huku.

2.Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Tillerson ametangaza kwamba siasa ya subira ya kimkakati ya Marekani kuelekea Korea ya Kaskazini imekwisha (Tillerson alisema katika mkutano na wandishi wa habari pamoja na mwenziwe wa Korea ya Kusini Yun byung-se huko Seoul: “Wacheni niwe wazi hasa, hakika siasa ya subira ya kimkakati imekwisha. Tunadurusu  idadi mpya ya hatua za amani na diplomasia. Uwezekano wa namna zote upo mezani…”)(Reuters, 17/03/2017). Hili linatiwa nguvu zaidi ya kwamba Marekani imeridhishwa kiasi fulani kuhusu Syria baada ya kuthibitika uwezo wa Uturuki kuwalazimisha wanamapinduzi kuusalimisha mji wa Allepo. Yaani kupungua kwa hatari kubwa kwa mapinduzi ya Syria – kama inavyohisi Marekani – kunaiwezesha kushughulika zaidi na Korea ya Kaskazini na hapo tena suala la Korea ya Kaskazini likawa kadhia nambari moja katika meza ya rais Trump baada ya kuwa suala la Syria ni kipaumbele kikubwa kwa uongozi wa Obama. Na Marekani haikuacha kutayarisha mipango yake kwa bahari ya China, ikawa inaidurusu mipang kadhaa ya kufanywa huku ikitayarisha waitifaki wake. Kwahiyo ukawa mvutano na Korea ya Kaskazini una sauti kubwa ndani ya Washington.  Na likawa tangazo la Marekani kumalizika kwa siasa ya subira ya kimkakati linaashiria uwezekano wa Washington kutumia utatuzi wa kijeshi kwa Korea ya Kaskazini. Matoke yake Marekani ikatangaza majibu ya kiuchokozi dhidi ya majaribio ya kijeshi ya Korea ya Kaskazini kwa maneno makali, miongoni mwao ni:
a-Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Tillerson kuitishia Korea ya Kaskazini kwa silaha za nyukila (Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson aliitisha Korea ya Kaskazini kutumia “Makombora ya kinga ya nyuklia” – nuclear deterrence – ili kuikinga Korea ya Kusini na Japan, haya ni majibu makali zaidi katika zoezi la mwisho la makombora ya Pyong Yang. Na Tellerson yeye na wenzake wa Korea ya Kusini na Japan wakatoa tamko akisisitiza humo kuwa Marekani “imedhamiria” kuikinga Tokyo na Seoul  hata kwa kutumia “Kinga ya Kinyuklia” – Nuclear deterrence…) (Russian Sputmik Agency, 17/02/2017).                                                                                                                                                                                                      b- Kitisho cha Marekani kuipa silaha za nyuklia Korea ya Kusini na Japan (Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tellerson, alitangaza mapema leo kwamba haondoi uwezekano wa utatuzi ambao utapelekea kudhihiri kwa silaha za nyuklia Korea ya Kusini na Japani. Na waziri hakuweka wazi katika mazungumzo kuwa ni kupeleka silaha za nyuklia za Marekani katika eneo hilo, au silaha hizi zitakuwa zinatoka katika milki ya Korea ya Kusini na Japani…) (Russian Sputmik Agency, 18/03/2017).
c-Maneno ya upeo wa uchokozi katika yale Trump aliyoikumbusha Korea ya Kaskazini ya idadi kadhaa za silaha za Marekani ambazo anaweza kuzitumia kuipiga (Rais wa Marekani alifafanua pia kuwa jana amewasiliana na rais wa China, Xi Jin Ping na akamtaka katika mazungumzo yaliyodumu kwa saa nzima kuwa afikishe kwenye masikio ya kiongozi wa Korea ya Kaskazini Kim Jong-un kwamba Marekani si tu ina meli za kubebea ndege za kivita bali ina mpaka manuwari za nyuklia”. Na akasema kwa ukali: “Haiwezekani kuiruhusu Korea ya Kaskazini kumiliki silaha za nyuklia. Hadi hivi sasa hawana njia ya kuwa na silaha za nyuklia, lakini watakuwa nazo…”) (Russia Today, 13/04/2017 likinukuu gazeti la “Wall street journal” la Marekani).
d-Kwa sababu ya kuongezeka kwa mvutano hivi karibuni baina ya Marekani na Korea ya Kaskazini, baada ya Pyongyang kutangaza kufanya  majaribio mapya ya makombora na yenye kuogopesha matayarisho yake ya jaribio la kinyuklia la sita, Marekani ikatuma nguvu kubwa za kijeshi zikiwemo za kuteketeza na meli za kubebea madege ya kivita karibu na Korea ya Kaskazini.(Msemaji wa Kamandi ya Marekani ya Bahari ya Pacific amethibitisha kwamba meli la kubebea ndege za kivta la Marekani Carl Vinson na ndege zake. Na pia ndege mbili za makombora ya kuteketeza (destroyers of missile launchers) na maroketi launchers imeeleka upande wa Korea ya Korea baada ya kutarajiwa kusimama Australia na kwasababu iliwekwa katika matumizi ya “Hatua za dharura”. Msemaji akaongeza kuwa kitisho cha kwanza katika eneo chanzo chake ni Korea ya Kaskazini kutokana na mpango wake wa makobora…) na makamo wa rais wa Marekani, Mike Pence siku ya Jumamosi tarehe 22/04/2017 alithibitisha jambo hili.  Aliwaeleza wandishi wa habari huko Sydney: (Kuwa meli ya kubeba ndege za kivita “itakuwa katika bahari ya Japan ndani ya masiku tu kabla ya mwisho wa mwezi huu” pamoja ndege mbili za makombora ya kuteketeza (destroyers of missile launchers) na maroketi launchers. Akaendelea “Ni juu ya serikali ya Korea ya Kaskazini kutofanya makosa kwani Marekani ina raslimali, waajiriwa na uwepo katika eneo hili la ulimwengu, mambo ambayo yanaruhusu kuhifadhi maslahi yetu na amani ya maslahi haya na amani ya washirika wetu”. Na Pence aliapa kwamba kutakua na “Majibu  ya kupindukia na yenye athari” dhidi ya shambulizi lolote kutoka Korea ya Kaskazini, huku akisisitiza kwamba nchi hii ina “kitisho hatari zaidi kwa amani na utulivu katika eneo la Asia na Bahari ya Pacific”) (France News Agency, AFP, 22/04/2017)
e-Mazoezi makubwa ya kijeshi ambayo Marekani inayafanya huko Korea ya Kusini, (Majeshi ya Korea ya Kusini na Marekani yameanza mazoezi makubwa ya kijeshi siku ya Jumatano ambayo hufanywa kila mwaka kwa ajili ya majaribio ya utayari wao kujilinda katika kukabiliana na vitisho vya Korea ya Kaskazin… Mazoezi haya yanafanyika katika wakati mvutano umeongezeka baada ya jaribio la karibuni la kombora la ballistic lililofanywa na Korea ya Kaskazini tarehe 12 Februari…) (Reuters, 01/03/2017). Na ni vyema kutaja kwamba jeshi la Marekani lina kambi kubwa ya kijeshi Korea ya Kusini yenye wanajeshi wa Kimarekani wapatao 28500 ambao ni sehemu ya kundi la wanajeshi katika nchi za bonde la China na visiwa vya bahari ya Pacific ambalo linakusanya zaidi wanajeshi robo milioni, ukiachilia mbali majeshi ya wanamaji waliopo baharini.

3-Mambo yako hivyo, Trump anatishia kana kwamba vita viko mlangoni…Isipokuwa kuna mambo yanaonesha kwamba Marekani haitaki vita hivi sasa, miongoni mwao ni:
a-Marekani ilitishia, ikaapa, na ikadhihirisha utayari wake kujibu kwa nguvu dhidi ya jaribio lolote jipya la Korea ya Kaskazini. Na Korea ya Kaskazini ikajibu kwa paredi kubwa la kijeshi tarehe 15/04/2017 lililorushwa na runinga ya Pyongyang. Ilionesha uwezo wa Korea ya Kaskazini wa kuvurumisha makombora ya ballistic kutoka kwenye nyambizi, na uwezekano wa kuwa baadhi ya makombora yake kuvuka mabara, yaani inawezekana kufika ardhi ya Marekani. Hapo ilidhihirika wakia ya nguvu hizi za Korea ya Kaskazini kuwa ni kizungumkuti kwa Marekani. Marekani inataka kupangavita bila ya kujipatisha udhia wowote au vita visiiguse ardhi yake,
Korea ya Kaskazini ilipodhihirisha hakika ya nguvu zake, uhakika wa vitisho vya Marekani ukawa katika kizungumkuti kikubwa. Na Pyongyang haikusita kwenye upeo uliyoyadhihirisha katika paredi la kijeshi na kurushwa na runinga, na hasa uwezo wa nyambizi zake kubeba makombora ya ballistic na kuyafyatua, bali ilifuatisha na jaribio la kombora tarehe 16/04/2017 nalo ni kana kwamba kombora lenye kuvuka mabara. Na hata ikiwa lilifeli ila lilizidisha ukaidi dhidi ya Marekani. Na ikadhihirika kwamba vitisho vya Marekani havikuwa vya kweli na kwamba Markani hivi sasa haiwezi kuvitekeleza, yaani Marekani bado haijawa tayri kwa vita…
b-Mpaka hivi sasa bado hakujapelekwa Korea ya Kusini mfumo wa makombora ya kinga ya “THAAD”, kilichopo ni matayarisho ya jambo hilo pamoja ya kwamba makubaliano yake yashapitiwa na mwaka (Msaidizi wa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani kwa mambo ya Asia ya mashariki na bahari ya Pacific, Susan Thornton, alisisitiza kwamba makombora ya kinga ya “THAAD” yatatumwa Korea ya Kusini kwa mujibu wa mpango uliowekwa. Na vyema kufahamu kwamba mifumo ya makombora ya Marekani ilikua maamuzi ya kuituma Korea Kusini ndani mwezi wa June au wa July ya mwaka huu.
Lakini kinachodhihirika ni kwamba Marekani na Korea ya Kusini zimeamua kulifanyia haraka jambo hili kutokana na jaribio la kombora la Korea ya Kaskazini. Na anaeleza kwamba makubaliano baina ya Washington na Seoul ya kutuma mifumo ya makombora ya “THAAD” Korea ya Kusini yalifikiwa mwezi wa July mwaka 2016… Na mipango hii ya kutuma makombora ya “THAAD” peninsula ya Korea inaishughulisha sana Urusi na China, wakati Japan inaona jambo hili linatia nguvu usalama wa eneo…(Russian Sputnik Agency, 17/04/2017)
c-Haitarajiwi Marekani kuingia vitani dhidi ya Korea ya Kaskazini kabla ya kutimia siku mia moja zilizowafikiwa pamoja na rais wa China kukamilisha makubaliano makubwa ya kibiashara ambayo yatadurusu mahusiano jumla ya kibiashara baina ya nchi mbili. Marekani inataka kudhihirisha ulaini katika biashara na China, kinyume na kile alichoahidi rais Trump katika kampeni yake ya uchaguzi ya kuzitoza kodi bidhaa za China 45%, yaani inajaribu kuirubuni Uchina ili kuishinikiza sana Pyongyang na kuwa kisingizio cha kuepukana nayo na kuiacha peke yake katika kukabiliana na Marekani na washirika wake. Jambo hili litaihakikishia Marekani malengo mawili:
KWANZA: Likifaulu hili, basi litaporomosha nafasi ya China kwa kudhihirika kuachwa na washirika wake. Na vilevile katika kuiporomosha nafasi ya China, rais Trump akatoa maelekezo ya shambulizi la makombora dhidi ya Syria tarehe 07/04/2017, Marekani imefanya hivi hali ya kuwa Trump yupo katika mapumziko ya chakula cha usiku huko Florida pamoja na rais wa China Xi Jinping. Jambo ambalo baadhi(ya wadadisi) wamelichukulia ni kuidhalilisha China. Al-Arabiya Net, 08/04/2017 imeeleza: ( Tovuti hii imemnukuu jenerali mstaafu, Jack Keane, ambae ni naibu wa baraza lililopita la maafisa wa ngazi za juu wa jeshi la Marekani, ikinukuu kutoka tovuti ya Fox News maoni yake juu ya kauli ya Trump: “Anatenda akisemacho… Hakika anapeleka ujumbe kwa Wachina”), yaani kuhusu azma yake ya kuipiga vita Korea ya Kaskazini, na kwamba China iishinikize Korea ya Kaskazini na iepukane nayo. Yaani ikifanya hivi, basi uwezekano wa mambo kuwa mepesi utapatikana katika maafikiano ya kibiashara…
PILI: Marekani inachokitaka katika kujaribu kudhihirisha karata ya China dhidi ya Korea ya Kaskazini kwa wingi wa kauli zake(Marekani) juu ya maafikiano ya nchi mbili kuhusu hali ya hatari ya Korea ya Kaskazini, kuwa jambo hilo liharakishe kufikia itifaki ya Marekani – Urusi, kwahiyo Marekani inaifanya karata ya Korea ni uwanja wa mashindano baina ya Urusi na China! Na kuongezeka kwa kauli hizi kumekuwa na mvuto… Mike Pence, makamo wa rais wa Marekani katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na waziri mkuu wa Australia, Malcom Turnbull, alisema: (“Tumehamasika kutokana na hatua zilizochukuliwa na China hadi hivi sasa”…Na wiki iliyopita Trump alisifu juhudi za China za kudhibiti kitisho cha Korea ya Kaskazini baada ya vyombo vya habari vya Korea ya Kaskazini kuionya Marekani juu ya shambulizi lisilotarajiwa…)(Al-Hayat Newspaper – Sydney Reuters, 22/04/2017)
d-Marekani inataka kuikabili Korea ya Kaskazini kwa eneo la nguvu ambalo litaidhoofisha Pyongyang, na eneo lenyewe ni kuliweka jeshi la Urusi ubavuni mwa (jeshi la)Marekani dhidi ya Pyongyang. Na huenda kama ilivyowekwa kama kiongozi wa vita nchini Syria. Jambo ambalo litakoroga sana hisabu za Korea ya Kaskazini inayodhania kwamba Urusi ni adui wa Marekani. Na mpango huu mpya wa mpango wa zamani wa Kissinger ambao umelenga vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi wakati wa utawala wa Obama. Na hadaa za utawala wa Trump kwa Urusi, Marekani imezichelewesha kuzifanikisha. Na suala lililokuwa muhimu katika ratiba ya kazi za waziri wa mambo ya nje, Tillerson huko Moscow tarehe 11/04/2017 ni ushirika dhidi ya Korea ya Kaskazini,na ndilo lililothibitishwa baadae na vyanzo(vya habari) kwa Russia Today tarehe 16/04/2017 kikinukuu kutoka gazeti la Kommersant la Urusi (“Ama kuhusu Marekani, kwa mujibu wa matokeo ya mazungumzo ya Moscow yaweza kuzingatiwa kwamba mjadala wa tatizo la Korea ni mafanikio. Na kwa mujibu wa vyanzo vya habari suala hili lilikuwa ni katika mambo ya kipaumbele ya ziara ya Tillerson huko Moscow.”). Na pindi vita ya Korea ikilipuka kabla ya maafikiano ya Marekani – Urusi, basi yawezekana Marekani ikaingia hasara kubwa. Kama vile ilivyo Marekani kuwa inapendelea kuifanya China iathirike kwa kuongeza vitisho ili ingilie Korea ya Kaskazini kwa hofu ya kuzuka vita vya nyuklia…
4-Juu ya yote hayo, Marekani hivi sasa haiko tayari kwa ajili ya vita dhidi ya Korea ya Kaskazini. Na haina suluhisho jengine munasaba, kwa hiyo inaisubiri China kushinikiza huku ikijaribu kuharakisha hilo. Na inazidisha kauli zake kwamba Marekani iko tayari kulitatua tatizo (hili) peke yake, yaani bila ya China. Na ni kana kwamba Marekani inaitisha China ili itii na kukubali kuishinikiza Pyongyang iachane na silaha zake za nyukila. Marekani vilevile inasubiri maafikiano yake na Urusi ili iyahusishe katika utatuzi wa kitendawili cha Korea. Ama masharti haya hayajatimia kwa ajili ya vita kwahiyo Marekani inarudi nyuma juu ya vitisho vyake, ijapokua Korea ya Kaskazini haijarudi nyuma juu ya majaribio yake ya makombora na nyuklia na inaendelea kutishia vita vikubwa vitakavyoifikia ardhi ya Marekani. Na inadhihirisha kuwa haiogopi vita vya nyuklia. Na dalili ya kurudi chini lugha ya Marekani ni yale yaliyomo katika kauli za hivi karibuni:
(Associated Press imenukuu chanzo cha kijeshi cha Marekani ambae hakutaka jina lake litajwe, kwamba Washington kwa sasa haijawa na nia yoyote ya kuishambulia Korea ya Kaskazini hata ikiendelea Korea ya Kaskazini majaribio yake ya kinyuklia na makombora. Na chanzo kikaongeza kwamba mipango ya Marekani haitabadilika isipokua Pyongyang itakapoilenga(kimashambulizi) Korea ya Kusini, Japan, au Marekani. Na kwamba uongozi wa Marekani kwa sasa umekubali kusubiri na kuacha kukuza mvutano…) (Russia Today, 15/04/2017). Na Marekani inakwenda mbio kupunguza zaidi mvutano ambao iliuleta yeye kwa kasi.  (Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Marekani alitangaza kwa wakala wa Mambo ya Mashariki Asia na bahari ya Pacifiki, Susan Thornton kwamba nchi haitoendeleza mzozo na Korea ya Kaskazini au kuiondoa serikali yake. Na pia Thornton katika mkutano na wandishi wa habari:
(“Marekani ilitangaza kwa uwazi kwamba inataka kutatua mzozo huu wa Korea ya Kaskazini kwa mpango wa kubwaga silaha za nyuklia kwa amani katika Rasi ya Korea. Na sisi kwa hakika  hatulitilii nguvu suala la mzozo au kuiondoa serikali”) (Russia Today, 17/04/2017). Na Makamo wa rais wa Marekani, Mike Pence ameeleza kwamba(Bado anaona inawezekena kwa Peninsula ya Korea kuachana na silaha za nyuklia kwa amani kwa jambo zuri jipya la Washington kuipa kazi Beijing. Na hayo, juu ya kwamba hofu inayoendelea kutokana na hatua ya Korea ya Kaskaziini kufanya majaribio mapya ya kinyuklia muda mfupi ujao. Pence akaongeza kwamba hakika tunaona ikiwa China na mataifa washirika katika eneo watatia shinikizo hili, basi ipo fursa ya kufikia lengo la kihistoria kwa kuifanya Peninsula ya Korea kuwa ya amani bila ya  silaha za nyuklia…) (Al-Hayat Newspaper – Sydney Reuters, 22/04/2017).
5-Hii hasa ndio hali ilivyo na mvutano katika Peninsula ya Korea, mambo yaliyosababishwa na mipango na ubabe wa Wamarekani. Na hizo ndizo pande zake za wahusika.  Na haya (yaliyoelezwa) ndio msingi jumla wa kuifahamu hali halisi… Hata hivyo, hali inaweza ikalipuka wakati wowote. Na kitisho cha kulipuka kwa vita huenda kinasubiri kukamilika masharti yake, hasa makubaliano baina ya Marekani na Urusi, na kama hazijaafikiana basi uwezekano wa mvutano kukua utazidi. Na ikiwa maafikino yao yatachelewa sana au yasifanyike kamwe, basi hali katika Peninsula ya Korea itabakia kuwa tete (ya kati na kati) kimvutano kwa lengo la kuendeleza shinikizo dhidi ya Pyongyang ili iachane na silaha zake za nyuklia… Ama uongozi wa Marekani ukiendeleza ubabe katika kuamiliana na Korea ya Kaskazini basi matokeo yake yatakuwa ni ya hatari sana… Kwani uongozi huu hauna hekima ya kutekeleza mikakati ipasavyo. (Waziri wa Ulinzi wa Marekani wa zamani Leon Panetta alionya Washington kuanza shambulizi dhidi ya Korea ya Kaskazini akisema kwamba hatua yoyote juu ya jambo hili inaweza kulipua vita ya nyuklia ambayo itateketeza roho za mamilioni“na hii ndio” sababu iliyowazuia marais wa Marekani waliopita kushinikiza kuifyatua silaha na kuipiga Korea ya Kaskazini. Na akaongeza: “Ni juu ya uongozi wa Marekani kuchunga juu ya kauli zake na kuepuka kukuza mvutano na ichukue hadhari pia isifanye maamuzi ya haraka” akiashiria umuhimu wa kuisubiria China itakachoweza kukifikia katika kutuliza hali. Hasa kwa kuwa Washington hivi karibuni imeipa fursa ya kuingilia kati yenye athari…) (Russia Today, 15/04/2017).
6-Ama msimamo wa China, ni kuwa inafahamu kikamilifu kwamba yeye ndie mlengwa kwa njia isiyo moja kwa moja kutokana na Marekani kuchochea mvutano ukiachilia mbali vita. Kwahiyo inafanya bidii  kuzima joto hili kwa wito wa utatuzi wa amani wa mzozo huu na inapinga utatuzi wa kijeshi na inapinga wazi wazi kuifanya Peninsula ya Korea ni ukanda wa kijeshi(militarization). Na katika hili ni kukataa kwa kauli moja kuwekwa nchini Korea ya Kusini mfumo wa makombora ya kinga wa “THAAD” wa kimarekani.(Na Wizara ya Mambo ya Nje ya China ikaeleza kukataa kwa Beijing kutumwa mfumo wa “THAAD” na wakati huo huo ikaitaka Korea ya Kaskazini na majirani zake kujizuia na vitendo vyovyote vya kiuchochezi…(Al-jazeera Net, 17/04/2017) Lakini inatarajia mabaya zaidi na inajitayarisha kwa uwezekano wa vita na ina wasiwasi wa hilo.

Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa China, Wang Yi alisema: “Vitakapozuka vita hakutakua na mshindi” (BBC, 15/04/2017). Ama maandalizi ya vita ya Uchina, limetajwa hili na Russia Today tarehe 14/04/2017 (limeweka wazi shirika la Habari la Marekani la United Press International kwamba majeshi ya China yamepokea amri kutoka kamandi kuu ya jeshi moja kwa moja kuendelea kuwa katika hali ya juu ya tahadhari katika maeneo matano ya kijeshi. Na kwa mujibu wa kituo cha Haki za Binadamu na Demokrasia ambacho si cha kiserikali cha Hong Kong, wakala hawa wakasema kwamba bataliani ya mizinga katika maeneo ya kijeshi ya Chongqing, Sichuan na Yunnan wameamriwa kwenda na kufunga kambi katika mipaka na Korea ya Kaskazini.
Na kwa mujibu wa kituo hiki (cha Haki za Binadamu) kiasi cha wanajeshi 25,000 kutoka kikosi cha 47 kilichopo upande wa magharibi wa nchi wameamriwa kutoka na zana zao za kivita kuelekea mbali upande wa kambi ya kijeshi iliyopo karibu na mipaka ya Korea ya Kaskazini. Kama lilivyoeleza shirika la kiuwakala la Japani kwamba sababu iliyopo ya majeshi ya China kupelekwa katika mipaka ya Korea ya Kaskazini ni wasiwasi wa Beijing juu ya uwezekano wa Washington kufanya shambulizi dhidi Pyongyang bila kutarajia, ambayo ni kama hali ya mashambulizi ya mizinga ya Marekani yaliyovurumishwa juu ya kambi ya kijeshi ya Al-Shayrat nchini Syria).
Haya ndiyo tunayoyaona yana nguvu katika jambo hili kulingana na uchmbuzi wa hali halisi iliyopo walau katika kipindi kifupi kijacho bali na zaidi ya hapo. Tunasema haya kwa sababu ulimwengu leo unatawaliwa na wanyama wenye vazi la binadamu, kwao damu ya watu haina thamani yoyote…  Ikiwa maslahi yao yatapelekea kumwaga damu basi watakimbilia kufanya hivyo mchana kweupe tena kwa silaha zao za kinyuklia na zisizo za nyuklia kama walivyowahi kufanya na wanavyoendelea kufanya…
Hakika ulimwengu hautokua na amani na usalama mpaka utakapoondoka ubepari na nidhamu nyengine zilizowekwa na binadamu na kukoma kutawala ulimwengu. Na hapo tena nidhamu ya haki na uadilifu, nidhamu ya Khilafa Rashida, nidhamu ya Mola wa ulimwengu, itatawala katika ulimwengu huu na itaeneza kheri, furaha ya maisha na utulivu. Kwani Muumba ndie anaejua maslahi ya viumbe wake;
“Tambueni kuwa yeye anajua alichokiumba na Yeye anajua yaliyofichika na yaliyowazi” (Al-Mulk:14.)
26 Rajab 1438 AH      23rdApril 2017 CE

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.