“Muqalid Mutabi’ Kwenda kwa Imam Annawawy

Swali

Assalamu alaykum…allah akulinde na akuhifadhi amiri na ndugu yangu, namuomba allah akujaalie muda ujibu swali hili.

Nasoma katika kitabu chako, Taysir AL-wusul ila Al-Usul [wepesi wa kufika katika misingi] (uk.273),kwamba:”swali lililojitokeza ni hili; kwa anaefanya taqlid (kufata kwa kuiga hukmu ya kisheria),kama atafata au kuiga jambo fulani, jee ataruhusiwa kumfata au kumuiga mtu mwingine katik hilo hilo ? Jibu la swali hili nikwamba muqalid(mfataji/muigaji) analazimika kufata sharia ambayo imefanyiwa utafiti na mtafiti (mujtahid) anaemfata. Hii inamaana kwamba: kama mfuataji atatekeleza sharia ya yule anaemfata katika jambo,hairuhusiwi kuacha kumfata anaemfata (mujtahid wake) na akaanza kumuiga au kumfata kwasababu sheria imeshamuajibisha katika kumfata yule wa mwanzo alieanza kutekeleza ijtihadi zake”. mwisho wa kunuuu.

Hivyo, swali lililokuja katika kichwa changu: #kwamfano, kama mjinga ambae hajui lugha ya kiarabu anafata sharia kutoka kwa imam shafi, allah amrehem (mfano katika swala) na anaifata, kisha akasoma hukmu ya sharia ya swala katika kitabu cha fiqh kilichotarjumiwa katika lugha ya kirusi na mujtahid mwingine(kwamfano imam malik, allah amrehem) mtu huyu akaisoma kwa lugha ya kirusi na akahitaji kuacha mtazamo wa hukmu au sharia ya imam shafi na akataka ashikamane na mtazamo wa ijtihadi za imam malik..swali langu hapa: Je inaruhusiwa kufanya hivyo hivyo katika sharia ? Katika maneno mengine, je anaweza kuipa nguvu dalili katika lugha nyingine kuliko(isiyokua) ya kiarabu ? Kwanini nauliza swali hili ? Kwasababu # Waislamu wengi katika mkoa wangu wanaacha rai au mtazamo wa mujtahidi ambae wamekua wakimfuata kisha hufata mujtahidi mwingine katika mambo yaleyale. Tena wakati huo huo hawana ujuzi wowote wa lugha ya kiarabu wala sayansi ya sharia! Wanasoma aya na hadith katika lugha ya kirusi na wanadai kwamba ni ushahidi wa kisheria! Tafadhali naomba unipe majibu kwani itasaidia mimi kuelewa na wengine pia. Allah akulipe kheri.

Wassalam alaykum.

 Jibu:

Wa Alaikum Assalam Wa Rahmatullah Wa Barakatuhu

Kama ifuatavyo:

Kama muislamu atafata au kuiga jambo fulani katika # madh-hab yoyote, mfano katika swala kutokana na madh-hab ya abuu hanifa,na akataka abadilike au abadilishe hilo na aswali kwa kufuata madh-hab ya imam shafii,kwamfano, hii inaruhusiwa lakini kwa kushkamana na haya yafuatayo:

  1. Kwamba jambo hili limeegemea katika nguvu za ushahidi wa kisheria na sio kwasababu nyingine ni nyepesi au inakubaliana na matamanio yake, kwani ni haramu kufuata matamanio,allah anasema.

فَلَا تَتَّبِعُوا الْهَوَى

“Hivyo msifate matamanio yenu”

An-Nisa: 135

Allah (swt) pia amesema:

فَإِنْ تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ

Na ikiwa mtazozana katika jambo lolote basi lirejesheni kwa allah na mteme.”

An-Nisaa: 59

Nikurejea katika sifa za nguvu ya ushahidi kwa muqalid (mfaataji) alizosisitiza allah( swt) na mtume (s.a.w), na hili lipo mbali na ufuataji wa matamanio,na kuchagua ijtahdi moja kati ya mbili bila kuzingatia nguvu ya dalili(#sharia) huko ndio kufata matamanio,ambapo pazuia kurejea kwa allah na mtume wake. Kuzipa nguvu sifa za dalili ambazo muqalid anachagua kati ya mujtahid mmoja na mwingine,zipo nyingi lakini muhimu zaid ni hizi: # ujuzi(elimu),uwezo wa uelewa/ufahamu na uadilifu(haki), hii ni kwasababu ya ushuhuda wake kwamba hizi ni hukmu za sharia hivyo nilazima zikubaliwe hilo lazima liwe limeegemea uadilifu wa mwalim anaemfundisha.uadilifu ni msingi wa kila mmoja ambae tunachukua hukmu za sharia kutoka kwake,vivyo hivyo,mujtahid na mwalimu haiwezakani kuwatenganisha.yoyote anaeamini kwamba imam shafi anaelimu na ujuzi na madhhab yake yapo sahihi, haitaruhusiwa kwake yeye kuchukua madhahab mengine kwa matamanio yake, isipokua aweza kuchukua hukmu tofauti kinyume na huyo aliemchagua baada ya kuhakikisha dalili nzito na yenye nguvu.hivyo uzito wa dalili hauepukiki, na hilo halitakiwi kuegemea katika matamanio ya mtu. Si sahihi kwa muqalid kuchukua rai au hukmu ya madh-hab katika kila jambo kulingana na anavyopendelea yeye.

2.kuna aina mbili za kupata elimu (ujuzi) katika #hukmu za kiislamu, mujtahidi na muqalid, na hakuna cha tatu.kwasababu uhalisia ulivyo mtu aweza kupata ujuzi (elimu) kupitia ijtihadi yake, au kile alichokifikia mwingine katika ijtihadi yake, na hili lina mipaka kwa haya mawili. Hivyo basi,kila mmoja ambae sio mujtahid basi atakua ni muqalid (mfataji) kwa namna yoyote, jaambo hili katika #Taqleed (uigaji/ufuataji) ni kuchukua hukmu kwa wengine bila kujali kama anaechukua  ni mujtahid au la. Haijuzu kwa mujtahid kuiga au kuwafata mujtahidina wengine katika jambo moja, hata kama anauwezo wa ijtihadi. Atakua ni muqalid katika jambo hili. Hivyo, rai inaweza ikachukuliwa na mujtahid au na mtu yoyote asiekua mujtahid.

  1. Mujtahid ni yule tu aliefuzu kufanya ijtihadi , kwakua na elimu au ujuzi toshelevu katika lugha ya kiarabu na elimu ya kutosha kuhusu naasikh na mansukh na sunnah na ujuzi wa kutosha wa namna ya kupima uzito wa dalili na uwezo wa kuvua hukmu.kama mujtahid atafanya juhudi katika jambo na akavua hukmu, haitakubalika kwake yeye kufata au kuiga mujtahid mwingine kwa jambo ambalo ni tofauti na# rai katika ijtihad zake.Hataruhusiwa kuacha rai yake au akaacha kuifata katika jambo hili isipoku katika hali fulani, muhimu nikwamba, ikiwa atafaham kwamba ushahidi alionao ni dhaifu, na aliokuanao mwingine una nguvu # kuliko ushahidi wake. Katika eneo hili, nilazima aachane na rai au hija zake haraka sana na achukue rai yenye nguvu. Itakua ni haram kwake yeye kubakia na ijtihadi yake katika hali hiyo.

Hili ni kuhusu mujtahid kama atafikia ijtihadi yake na hiyo ijtihad yake ikamuongoza katika hoja fulani katika jambo. Vyovyote iwavyo, kama mujatahid hakufanya ijthad katika jambo,basi niruhusa kwake kumfuata mujtahid mwingine yoyote na hataruhusiwa kufanya ijtihad katika jambo hilo, kwasababu ijtihadi ni faradhi kifaya(kuwakilishana) na sio lazima kwa kila mmoja, Hivyo kama anafahama hukmu ya sharia katika jambo fulani, mujtahid halazimikiwi kufanya ijtahad katika kaika hilo, Lakini inaruhusiwa kwake kufata mujtahidina wengine katika mambo, Hivyo ndivyo mujtahid aweza kuhama kutka katika # rai moja kwenda nyingine kwa kuzingatia uzito wa dalili, ambao umetiwa nguvu kwa ushahidi, bila kujalisha yeye ni katika waliofanya ijtihad na kuvua hukmu au ni wengine.

  1. Huu ndio uhalisia wa ufataji au uigaji wa mujtahid. Kwa wale wasiokua mujtahidina, wapo katika aina mbili: muttabi’i na A’mmi na kila mmoja wao ana mashart ya uhamaji wa madh-hab kutoka dheheb moja kwenda jingine, na uhamaji huu haugemei katika kufata matamanio, au uwepesi bali ni kwa kufata hukmu za sharia kwa mutabii na ammi,

-Muttabii ni yule ambae anautambuzi katika sharia,zaid ya hayo ni

This is the reality of the imitation of the Mujtahid. As for the non-Mujtahid, they are two types: Mutabi’ and A’mmi and each of them has conditions when moving from one school of thought to another, and this transition in all cases is not based on desire, convenience, or ease, but by following the Shariah criteria of outweighing for the Mutabi’ and for the A’mmi,

  1. Anaujuzi mzuri wa kiarabu, anauwezo wa kufaham kiarabu katika jambo lolote, na anauwezo wa kusoma qur-an kwa kiarabu. Na anauwezo wa kuelwa hadthi kwa kiarabu, hili halimaanish kuelewa kila neno lakin aweza kuuliza na kuelewa maana yake.
  2. Kuweza kuwa na ujuzi wa kutafsiri kuelewa mutawatir,sahihi,hassan, hadith dhaifu na kuwa na ujuzibwa kufaham vitabu sahihi. Kwamfano, akiona hadith katka bukhar #muslim, anajua hiyo ni sahihi, na kama akisoma hadith katika tirmidh, na tirmidh amesema hadith hiyo ni hassan, awe ajua maana yake…hivyo awe na uwezo wa kugundua hadith sahihi, hassan,dhaifu na nyinginezo

Na mutabii hutoka katika rai moja kwenda nyingine kwa kujua ushahidi. Atafata hukmu ambayo anajua ushahid wake kuliko hukmu ambayo hafaham ushahid wake, kama atafata madhhab. Kama atafata au kuiga rai bila ujuzi au ufaham wa dalili zake, na anafaham rai nyingine,akafata rai yake, Bila kujua dalili yake, na akaona madhhab mengine ambayo afaham dalili yake, atafata vile ambavyo ajua dalili zake na ataacha asioijua ushahidi wake.

-Ammi ni yule asiejua hukmu ya sheria.hana ujuzi wa lugja ya kiarabu na hana ujuzi wa dalili za qur-an na sunnah…na anamuabudu allah kama vile shekh alivyosema katika madhhab. Mtubhuyo hawezi kuhama kutoka madhhab moja kwenda nyingine katika jambo lolote, bila kujali uzito wa dalili au la. Atafungamana na dheheb moja analofata, hivyo atamfata imam wa msikiti katika namna ya usomaji wa qur-an. Hivyo atawasali kama wao  kwamfano katika hili hawez kuhama kutika rai moaja kwenda nyingine isipokua kwa uzito wa dalili ambao atafaham mtu mjuzikuliko wale anaowaamini.Ambao anafaham uadilifu wao. Ikiwa mtu huyu anaabudu kulingana na abuu hanifa basi itakua hivyo na ikiwa watahama wale anao waamini na yeye atahama….

Kwamaneno mengine, ammi anahama kutoka rai moja kwenda rai nyingine kwa uzito wa dalili.

Pindi ammi akijua mtu anaemuamini katika uchamungu na uadilifu,na akawa na hakika kwa ujuzi wake anaweza akamfata mtu huyu katika madhhab yake.

  1. Hii ni katika hali pindi mtu akifata mujtahid au anahitaji kubadilisha mujtahid, atahitajia dalili za kisheria, hata pindi akiwa na elimu au ujuz wa dalili, kama anamfata mujtahid au bila ujuzi wa dalili.au amesoma kutoka kwa mtu mwingine ambae anaamini ushahid wake unanguvu kuliko anaewafata.Lakini ikiwa hakumfata mujtahid katika jambo la mwanzo na kuamua kuwa muigaji kwanzia muda huu basi atamfata mujthid ambae anauhakika nae kwa muongozo wake na ujuzi wake.Nibora kutaja kwamba uigaji katika jambo moja lazima uwe ni kutika kwa mujtahid mmoja katika jambo hilo kwa kufata kanuni na misingi yake…kwamfano,swala lazima ichukuliwe kutoka kwa mujtahid mmoja kwa kuzingatia kanuni na mising yake..pia vivyo hivyo katika Udhu,kisimamo na rukuu..vyotr hivyo vichukuliwe kutok kwa mujtahid mmoja, na sio kuchukua swala kwa abuu hanifa na udhu kwa imam shafii.Lakini katika mambo tofauti, mfano swala, swaumu na hajji inaruhusiwa kuchukua yote hayo kwa mujthid mmoja,kuchukua swala kwa mujtahid mmoja na swaum kwa mujithid mwingin na yasiokua hayo.

6.kwa kuegemea ushahidi wa hapo juu,jibu la swali lako kuhusu # ndugu ambao hawajui kiarabu na hujichukulia kwamba wao ni mutabi’ na hivyo husoma ushahidi wa tafsiri, na hivyo wanahama kutok madhhb moja kwenda nyingine kana kwamb wao ni muttabii’ wafuataji ambao wamekinaika baada ya kujua ushahidi…uhalisia wao huashilii hilo, kwasababu hawajui kiarabu, hivyo tarjuma zao hazitoshi kuhama kutok madhhab moja na kubadili nyingine.Lakini wanapaswa kufahama kwanz dalili nzito za kisheria kama kujua mtu wanaoweza kumuamini ambae kupitia yeye wanaweza kujua kiarabu,mtu ambae anaweza kuwasomea dalili kwa kiarabu na kuzielezea na kuwaonyesha ni madhhb gani ambayo ni mdhubuti..kama watathibitisha kupitia ujuz wake na ufaham wake basi itaruhusiwa kuhama madhhab kwa kuteemea imani juu ya huyo mtu…hivyo ikiwa ndugu hao wanahitai kuhama kutoka madhhb ya awali kwenda mengine haitoshi kusoma tarjuma maadam hawajui kiarbu, ila wanalazimika kuwa ushahidi wenye nguvu wa Amm katik toleo la tarjuma.

Hivi ndivyo nijuavyo katika swala hili na allah anajua zaidi.

Ndugu yako,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

15 Jumada Al-Awla 1439 AH

1/2/2018 CE

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!