Rais Erdogan wa Uturuki Asema Tatuo la Changamoto za Waislamu wa China Linawezekana

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari:
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki hivi karibuni ameuambia utawala wa china kwamba kinachofanywa kwa waislamu wa Uighur ni udhalilishaji mkubwa wa ubinadamu

Rais wa Uturuki Recep Tayyib Erdogan alisema suluhisho lipo la kuwasaidia waislamu wanaoshikiliwa katika kambi maalum”akizungumzia uwajibu wa pande zote, katika nukuu zilizonukuliwa siku ya jumatano.Uturuki ni nchi pekee yenye waislamu wengi kuipinga chini hadharani kuhusu ushikiliaji wake wa waislamu katika kambi hizo maalum na inakadiriwa jamii hii ya Uighurs inamiaka milion moja pamoja na waislamu wengine wa jamii za wachache katika eneo la Xinjiang.

Lakini Erdogan alikua mlaini sana baada ya kukutana na rais wa china Xi Jinping mnamo siku ya jumanne katika jiji la Beijing. “Naamini tunaweza kufikia muafaka katika jambo hili kwa kuzingatia kila upande” Erdogan aliwaambia waandishi wa habari Beijing kabla ya kurudi Uturuki.

Beijing imeongoza kampeni katika eneo la Xinjiang kufuatia msururu wa mashambulizi ya visu na machafuko ya kikoo kwa zaidi ya miaka 10. China imekua ikikataa kushikilia watu kinyume na matakwa yao kwa kusema kwamba ni” vituo vya mafunzo”ikilenga kuwaondoa “magaidi “miongoni mwa raia.
Wizara ya mambo ya nje ya uturuki mnamo mwezi wa pili ilishutumu china namna inavyowashughulikia watu wa Uighurs kwa kusema “ni udhalilishaji mkubwa wa ubinadamu”. (Aljazeera.com)

Maoni:
Mnamo 24 Julai 1924, Lord Curzon, aliekua ni waziri wa nje wa Uingereza ,alitangaza katika House of Commons, “…kwamba Uturuki (makao makuu ya Khilafah) imeanguka na haitaweza kuinuka tena kwa sababu tumeangamiza mfumo wake wa kimaadili, wa khilafah na uislamu.”

Uturuki inalenga zaidi kuhifadhi undugu wa kiuchumi na china kuliko kujali hali za waislamu wa Uyghurstan. Kitisho zaidi ni ukimya wa viongozi wetu ambao wamekua na furaha kusimama kwa miguu ya Trump, kutumia mabilioni ya dola za wananchi kwa kuuwa wenyewe nchini Syria ,Yemen na Libya. Vibaraka ,wanapoteza utajiri wetu kwa wamagharibi kwa kuwatengenezea silaha za kutufanya kuendelea kuwa watumwa na kuwapa fursa zaidi wamagharibi katika uchumi wetu.

Uturuki kama nchi nyingine, zimeachana na njia ya Rasulullah (saw) na imewekwa katika njia ya “ukafiri na utwaghuti” .Tumegawanywa na kanuni za kijahiliyya zilizoingizwa katika ummah ambazo hazina uwezo wa kuondoa matatizo ya ummah, iwe ni Uyghurstan au sehemu nyingine yoyote katika dunia. Uturuki haiwezi hata kujisaidia yenyewe kutoka utegemezi wa kiuchumi wa magharibi. Imetegwa katika nyuzi za buibui, ukafiri umetamalaki kwao, hawana mashiko ya kiitikadi wala kielimu wanahangaika kutafuta suluhu la kiuchumi, kisiasa na hata matatizo ya kijamii kutoka kwa mjenzi yule yule anaefanana na mmagharibi.

Tunaijadili China kama vile ilivyo kwenye habari, ipo vile ambavyo magharibi inavyotaka tuione. Uhalisia wetu ulivyo ni kwamba waislamu wanaendelea kunyongwa kote katika dunia, na magharibi inaendelea kuficha hali hii na kuonyesha hali tofauti katika nchi zetu kuanzia Malaysia, Sudan hadi Misri, Palestina na Iran. Viongozi wetu wanasujudia magharibi , kutabikisha ukafiri na sheria za kitwaghuti juu yetu. Jambo lisiloshangaza hata baada ya uhuru tumebakia tumegawanywa, kutumikishwa na wakoloni na kushindwa kuungana, ili kufanya majibu ya wale waliotuvamia na kutuua, na hivyo tumeshindwa kujikomboa ukombozi wa kweli.

Karne ya 21 CE inaonyesha ummah wa kuislamu unvyoteswa, utumwa na kugawanywa.

Hakuna mpango mkakati utakaowezekana bila muundo wa kinguvu ambao unaruhusiwa katika uislamu ambao unatakiwa kuwepo kwa ajili ya kuandaa na kuzuia madhara kwa ummah wa kiislamu ikiwa ni pamoja na kuulinda ubinadamu kutoka katika unyonyaji wa wakoloni wa kimagharibi. Rasulullah (saw) ameweka hili wazi kwamba ulinzi ni jukumu msingi linalotakiwa kubebwa na Ameerul Mu’mineen. Abu Hurairah (Radhiallahu Anhu) amepokea kutoka kwa Rasulullah (saw) kwamba,

«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ فَإِنْ أَمَرَ بِتَقْوَى اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ وَعَدَلَ كَانَ لَهُ بِذَلِكَ أَجْرٌ وَإِنْ يَأْمُرْ بِغَيْرِهِ كَانَ عَلَيْهِ مِنْهُ»
“Kiongozi ni kama ngao ambae amri zake ni lazima zitiiwe pindi waislamu wakipigana, hapo ndipo watakiwa kukimbilia kama ngao yao. Na kama atakua na khofu ya Allah na akatenda wema,basi atalipwa , lakini kama atafanya kinyume, atakua na mzigo wa dhambi.”

Sasa basi, hatutafuti haki wala ulinzi kutoka kwa wale wanaotudhuru, bali tunatafuta radhi za Allah (swt) na yeye ameweka hili wazi kwamba waumini wanatakiwa kuishi kwa kufata uislamu pekee, na sio kufata kanuni na sheria za wakoloni.

(وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ)
“Hukumu baina yao kwa kile alichoteremsha Allah na usifate matamanio yao na kuwa makini wasikuvute ukaacha baadhi ya aliokuteremshia Allah” [T.M.Q. 5:49]

Imeandikwa na kituo cha ofisi ya habari Hizb ut Tahrir na
Muhammad Hamzah

Kwa hisani: http://www.hizb-ut-tahrir.info/…/20…/news-comment/17788.html

Maoni hayajaruhusiwa.