Swaumu (funga) na Khilafah zote ni Ngao

بسم الله الرحمن الرحيم

Swaumu ( ﺻﻴﺎﻡ funga) imefananishwa na ngao, inatulinda kila mmoja wetu na moto wa Jahannam. Mtume wa Allah (saaw) amesema « ﺍﻟﺼِّﻴَﺎﻡُ ﺟُﻨَّﺔٌ ﻣِﻦَ ﺍﻟﻨَّﺎﺭِ ﻛَﺠُﻨَّﺔِ ﺃَﺣَﺪِﻛُﻢْ ﻣِﻦَ ﺍﻟْﻘِﺘَﺎﻝِ » “funga ni ngao dhidi ya moto kama ngao ya yoyote kati yenu katika mapigano.” [Ibn Maajah]. Hivyo, katika mwezi wa Ramadhan, tunatekeleza faradhi ya kufunga kwa ajili ya kupata malipo makubwa kwa Allah (swt), msamaha wake, na huruma zake na kutafuta kila jema. Pamoja na hayo, Khilafah (Caliphate) pia imenasibishwa na ngao, sio kwa sisi, kama mmoja mmoja bali kama ummah kwa pamoja. Mtume wa Allah (saaw) amesema, « ﺇِﻧَّﻤَﺎ ﺍﻟْﺈِﻣَﺎﻡُ ﺟُﻨَّﺔٌ ﻳُﻘَﺎﺗَﻞُ ﻣِﻦْ ﻭَﺭَﺍﺋِﻪِ ﻭَﻳُﺘَّﻘَﻰ ﺑِﻪِ » “kwa hakika imamu (khalifah) ni ngao, mnapigana nyuma yake, na kwa kupitia huyo mnajihifadhi.” [Muslim]. Zaidi,fardhi hii sio hukmu ya sheria pekee bali ndio msingi wa utabikishaji uislamu, hivyo ni lazima kuilingania na kuilinda.

Kwa hakika, baada ya zama za Mtume wa Allah (saaw),  Khilafah ilikua ni ngao kwa ummah dhidi ya maadui zake. Hata kwa kipindi cha Ramadhani, dola ya kiislamu ilikusanya majeshi na kupata ushindi mkubwa , na kuwashinda waliokua maadui nguli. Katika mwezi wa Ramadhani 13 AH, Khilafah iliishinda dola ya Kiajemi katika vita vya Buwayb, na kuitikisha katika msingi wake na kupelekea  kuiangusha. Ramadhan 92 AH,  Khilafah iliifungua Andulusia (Spain), iliifungua ulaya na kutawala kwa karne nyingi. Ramadan 92 AH, Muhammad bin Qasim aliifungua bara hindi na kuingiza uislamu , na kujenga msingi wa uislamu dhidi ya washirikina wa kihindu kwa karne nyingi . Ramadhan 223 AH, Khilafah iliifungua Amooriyah (Amorium), pamoja na kwamba ilikua ni eneo muhimu kwa dola ya Kiroma. Ramadhan 658 AH,  Khilafah ilimshinda Tartars wa Ein Jaloot, ingawa alikua ameshachukua sehemu kubwa ya dola ya kiislamu. Baraka zote hizi wakati wa mwezi wa Ramadhani zilikuwepo katika zama zote , waislamu walijawa na ghera ya kutaka kutabikisha uislamu, kuufanyia ulinganizi na kuilinda.

Pamoja na hayo, bila ya ngao yetu  khilafah, majeshi yetu hayataweza kuukomboa Masjid al-Aqsa kutoka katika mikono dhalimu ya dola la kiyahudi na haitawezekana kusaidia waislamu wa kashmir kwa kuuliwa kwao na kujeruhiwa na kupofuliwa na washirikina wa kihindu. Zaidi ya hayo, badala ya kukusanya majeshi kwa ajili ya ulinzi wetu bali viongozi wanakusanya majeshi  kuwalinda viongozi wanotawala kwa ukafiri na kuchukua ardhi. Ramadhan hii, kama ambavyo viongozi wa kiarabu wanavyowasujudia watawala wa kiyahudi chini ya kivuli cha “ukawaida” basi ndivyo ambavyo viongozi wa Kipakistani wanavyowasujudia dola ya kihindu, huku wakitaraji mazuri kutoka kwa mabwana zao wa  Washington. Viongozi wa Pakistan wanafanya kazi usiku na mchana kufanikisha mazungumzo ya  utamaduni, uchumi, jeshi na kisisasa na dola ya India. Na kuwazuia waislamu wanapotaka ukombozi wao. Kwa hakika, utawala wa Bajwa-Imran unachimba kaburi kwa ajili ya usalama wetu, kwa kutaka kutabikisha fikra za kihindu za “Akhand Bharat,” (Greater India), kama viongozi wa kiarabu walivyoweka msingi wa“Eretz Israel” (Greater Israel).

Ramadhan hii, waislamu waiendee funga kama faradhi na khilafah kama faradhi.

Imeandikwa na ofisi ya kituo cha habari cha Hizb ut Tahrir na

Musab Umair – Pakistan

(Imefasiriwa kutoka kingereza)

http://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/site-sections/articles/khilafah/17326.html

Maoni hayajaruhusiwa.