Taarifa Ya Kuzuiwa Kongamano Na Serikali

Hizb ut-Tahrir Tanzania kwa masikitiko makubwa inapenda kuwaarifu waalikwa wote katika Kongamano la Kukaribisha Ramadhani lililokuwa lifanyike kesho Jumamosi tarehe 20 Mei 2017, Hoteli ya Mayfair Mikocheni, Dar es Salaam kwamba kongamano hilo limezuiwa na serikali.

Polisi bila ya hoja wametoa waraka ulioandikwa leo tarehe 19 Mei 2017 na tumepokea nakala yake usiku huu wakidai kuwa kongamano hilo ni kikao cha siri chenye viashiria vya kutokuwa na malengo mazuri katika jamii.

Tunauliza kikao cha siri kitafanywa katika ukumbi wa hoteli unaochukuwa zaidi ya idadi ya watu 450 ?

Au kikao cha siri kitaalikwa watu mbali mbali wakiwemo Masheikh, Maimamu, Wasomi, Wanasiasa, Wanahabari , Wanasheria, Wanaharakati, Wanamichezo nk ?

Na zaidi kikao cha siri hutangazwa katika tovuti na ndani ya mitandao ya jamii wazi wazi?

Tunachukuwa fursa hii kuwashukuru wale wote waliopokea mwaliko wetu na pia kuwaomba radhi kwa usumbufu nje ya uwezo wetu. Ukipata ujumbe huu mfikishie mwenzako.

19 Mei 2017
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut-Tahrir Tanzania.

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!