Ufafanuzi Kuhusu Janga la Corona

بسم الله الرحمن الرحيم

Nukta muhimu katika kufafanua janga la Corona.

1- Corona ni janga la kimaumbile aliloleta Allah Taala, kwa mujibu wa vyanzo vya habari na ufuatiliaji wa matukio. Japo hatuwaweki mbali dola ya Marekani na Uchina kuweza kusababisha janga hili. Lakini matazamo na rai yenye nguvu katika hilo ni tukio llilojiri kimaumbile

2-Sio sawa kuwafungia watu majumbani na kufunga shughuli zote za kimaisha na kusimamisha uchumi na maisha kwa jumla. Bali dola zimeshindwa kuamiliana na janga hili. Na lau wangechukua tahadhari za tangu mwanzo, na wagonjwa wakazuiliwa katika maeneo yao, maradhi yasingeenea, na walio wazima wangeruhusiwa na kuendelea na maisha ya kawaida

3- Kusimamishwa swala za Jamaa na Ijumaa misikitini sio sawa, kwa kuwa swala ya jamaa inasimama kwa uchache watu wawili, Imamu na muadhini wake. Na Swala ya Ijumaa inaweza kusimama kwa uchache watu 3. Hivyo, zingechukuliwa tahadhari na kupimwa maradhi wanaoingia Misikitini japo ni wachache, lakini Misikiti isifungwe,

Kinachosikitisha ni watawala katika miji ya Kiislamu wamekuwa kila Jambo linalsemwa na wakoloni wao wanafuata moja kwa moja.

(Ufafanuzi kutoka Sheikh, Mujtahid, Ataa bin Khalili (Allah sw Amuhifadhi) ambaye pia ni Amiri wa Hizb ut Tahrir)

Maoni hayajaruhusiwa.