Ujumbe wa Ameer wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah kwa wenye kuzuru machapisho yake kwa tukio la kufikiwa na Eid al-Fitr iliobarikiwa Mwaka wa 1438 Hijria/2017 Miladi

Sifa njema ni zake Allah (swt) na Sala na salamu zimfikie Mtume (saw), Familia yake, masahaba zake na wote wanaomfuata…

Kwa Ummah wa Kiislamu uliotukuzwa na Allah (swt) aliposema:

كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ

Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu” [Aali-Imran: 110]…

 

Kwa wabebaji da’awa wasafi na wachamungu, na hatusifu mtu yeyote kwa Mwenyezi Mungu, wale ambao husema maneno bora na kufanya kazi njema, ambapo Mwenyezi Mungu huwasifu wale ambao wana sifa hizo:

[وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِين]

Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu? [Fussilat: 33]…

Kwa wageni watukufu wenye kuzuru kurasa za wavuti, kuzipitia kwa uaminifu na ukweli na kwa wale wanaotafuta mema ambayo zimebeba kurasa hizi, Allah awalipe kwa yalio bora zaidi …

 

Kwa hawa wote, nawapa pongezi kwa Eid al-Fitr na namuomba Allah (swt) akubali Swaum zao na Qiyam na kuwafanya miongoni mwa waliokombolewa katika mwezi huu Mtukufu. Na pia namuomba Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu kwamba hii Eid iwe mwanzo wa baraka na ustawi kwa Waislamu ili tuweze kufurahia Eid zifuatazo chini ya kivuli cha Rayah ya Khilafah Rashidah, bendera ya ‘La Illaha Illah Allah Muhammadan Rasul Allah’, na kwa kweli hiyo sio ngumu kwa Allah …

 

Mwishowe nawatolea salaam na kuwaombea uzima wenu, Mwenyezi Mungu awatakabalie matendo yenu na awahifadhi kutokana na madhara na maovu yote.

[فَاللَّهُ خَيْرٌ حَافِظًا وَهُوَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ]

“…Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mbora wa kulinda, naye ndiye Mbora wa kurehemu kuliko wenye kurehemu wote. [Yusuf: 64].

Usiku wa Eid, 1 Shawwal 1438 Hijri / 25-6-2017 Miladi

 

Ndugu yenu,

Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!