Unyonyaji wa Rasilimali kwa Chaka la Miradi ya Maendeleo

Habari:

Vyombo vya habari vimeripoti ziara ya karibuni ya tajiri Bill Gates nchini Tanzania, ambapo taasisi yake ya Bill & Melinda Foundation ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 777 kufadhili miradi ya maendeleo katika kilimo, afya na nyanja ya mawasiliano ya kimitandao.

Maoni:

Taasisi ya Bill and Melinda ilitangaza kwamba msaada wao unalenga kupunguza vifo vya watoto, kutokomeza malaria, kupambana na utapiamlo, kutoa msukumo katika uzalishaji wa malighafi, kuboresha shughuli za ufugaji, na kuweka mfumo wa kisasa katika teknolojia ya mawasiliano. Hata hivyo, mara nyingi malengo ya misaada na ufadhili kwa nchi zinazoendelea ni jambo la kutiliwa shaka. Masuala ya misaada na ufadhili vina historia ndefu tangu karne ya 19 ambapo daima huambatana na shinikizo la kiuchumi/kisiasa kulazimisha nchi zinazoendelea kulipa fadhila.

Mashirika ya kibepari, makampuni na taasisi zao mara nyingi huwa na ajenda za kibepari nyuma ya pazia. Pamoja na madai yao kwamba dhamira ya msaada yao ni kutoa msukumo wa maendeleo na kwa misingi ya ubinadamu. Ukweli wa mambo, hilo ni kinyume kabisa na uhalisia.

Misaada na ufadhili wa huduma za kibinadamu vimekuwa vikitumika kama vyombo vya kisera kumakinisha unyonyaji wa rasilimali. Na kwa hakika misaada imevuruga kabisa jitihada dhaifu za nchi zinazoendelea kujiinua kimaendeleo kwa siku za usoni.

Ama kuhusu bwana huyu Bill Gates, tayari amekwishazuru Tanzania mara kadhaa bila ya kuripotiwa na vyombo vya habari. Wakati mwingine malengo ya ziara zake yakibainishwa wazi na mengine hayabainishwi. Bill Gates amekuwa akitafiti kwa upana barani Afrika kwa muda miaka 15 sasa. Katika ziara yake nchini Afrika ya Kusini (kabla ya kuja Tanzania) alitangaza kuwekeza kiasi cha dola bilioni 5 barani Afrika katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Ukichunguza kwa makini asili na malengo ya mabepari, hapana shaka utaona kwamba rasilmali za Tanzania zinazidi kuwa hatarini na ndio mlengwa mkuu, na kama kawaida ya unyonyaji inachoambulia nchi (changa) ni mirahaba duni na kodi hafifu.

Tanzania, Afrika ya Kusini na nchi zinazoendelea kwa ujumla zinahitaji dola yenye nguvu na huru, bila ya shaka ni dola ya Khilafah kwa manhaj ya Utume. Dola hiyo ndio inayoweza kudhamini kutumika vyema na kwa uadilifu rasilmali zote kwa ustawi  wa raia  wake,  na  sio kwa maslahi ya unyonyaji wa kibepari.

Imeandikwa na Ramadhan S. Njera

Mwanachama wa Ofisi ya Habari

Hizb ut-Tahrir Tanzania

Kwa ajili ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!