Utumwa

Katika biashara ya utumwa nchini Marekani kulikuwa na magroup mawili ya watumwa. Watumwa wa majumbani (house nigger) na watumwa wa mashambani (farm nigger). Watumwa wa mashambani walikuwa wanaishi maisha magumu sana na yenye udhalili mkubwa wakifanya kazi usiku na mchana. Ama watumwa wa majumbani walikuwa wakijiona wao ni bora kuwa wao ni tabaka la watumwa wenye hadhi kubwa. Kwani wao walikuwa wanakula mabaki ya vyakula vya Mabwana zao na wanavaa nguzo zao kongwe (mtumba) huku wakifanya huduma zote za ndani Katika majumba ya Mabwana zao.

Na pindi waliokuwa wanakutana na watumwa Wenzao wa mashambani na kujadili namna ya kupata uhuru wao kutokana na utumwa. Basi watumwa wa majumbani walikuwa hawakubaliani mikakati hiyo. Na walikuwa wakiharakisha Kupeleka taarifa kwa Mabwana zao juu ya mikakati ya ukombozi inayofanywa na watumwa wa mashambani. Na Mabwana hao walikuwa wakija na kuzipindua harakati hizo na kuwaadhibu vikali watumwa.

Sura kama hii hii ndio inapatikana katika ulimwengu wa kiislamu. Pale ambapo waislamu wenye kufahamu vyema Uislam wao, kuwa ni dini ya kimfumo yenye serikali kamili. Na Ummah wa kiislamu unapaswa kuishi maisha kiislamu na maisha hayo hayawezi kupatikana bila ya uwepo wa dola ya kiislamu ya kiulimwengu khilafah.

Kunapatikana kundi lingine ndani ya waislamu imma kwa sababu ya kuwa na maisha mazuri kama wajionavyo wao au kuwa na kazi fulani inayomuingizia kipato. Au anafanya kazi Katika serikali hizi za kidemokrasia basi wao ndio wanakuwa kuzuizi kwa Kurejea dola ya kiislamu ya khilafah. Na wao ndio wamekuwa ni majasusi wa wamagharibi dhidi ya waislamu wenye kutaka kurejesha maisha ya kiislamu kwa kuurejesha serikali ya Kiislamu ya kiulimwengu khilafah. Na wengine wanaonekana kwa sura ya nje ni waislamu Wazuri tu. Wengine ni wasomi kabisa…….

Watu wa namna hii nawakumbusha kuwa lengo la kuumbwa ni kufanya ibada. Na kufanya ibada sio kuswali kufunga, hijja sadaka na ibada mbili Tatu. Bali ibada ni kufuata sheria zote za Allah. Na hilo haliwezi kufanikiwa Isipokuwa kwa uwepo wa dola ya Kiislamu khilafah. Na kurejesha dola ya kiislamu ndio sunnah namba mmoja.

Lakini Wale wapinzani wa Qur’an na sunnah wa Mtume Katika waislamu hali ya kuwa wanajua na wakumbusha maneno ya Allah pale aliposema:

فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَنْ تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

“Watahadhari wale ambao wanakwenda kinyume na amri zake isije ikawafika fitna na ikawafika adhabu iumizayo”
[Surat An-Nur 63]

Uislamu umekuja kuwatoa watu kwenye utumwa wa kuwaabudu watu au sheria zilizotungwa na watu na kuwaongoza Katika kumuabudu Mola wa watu na kufuata sheria zake.

Sheikh Khatibu Imran Abuu Khaliil
Mwanachama wa Hizb ut Tahrir

Maoni hayajaruhusiwa.