Waachiwe Huru Sio Magaidi

0

Wakati tukiwa katika kumi la mwanzo la mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa kheri, maghfira na Rehma, tusisahau kwamba mwezi huu pia ni kielelezo cha mapambano makali baina ya haki na batil. Mapambano ya zama na kaumu zote tangu iumbwe dunia na mpaka mwisho wa saa.

Ramadhani inadhihirisha waziwazi kuwepo mgongano baina ya haki na batil. Ndani ya mwezi huu tunatakiwa na Muumba wetu kupambana kwa kujizuilia na kujidhibiti nafsi zetu, tukiandaliwa kwa ajili ya kumtumikia Muumba wetu na  kuilinda haki tunayoibeba dhidi ya batil.

Aidha, mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ambao ndio ulioshuka Quran na kuanza kupewa wahyi Mtume wetu SAAW ambao licha ya kuwa ni Rehma na ukombozi kwa walimwengu wote, lakini ulipata upinzani mkali na wa kutisha kutoka kwa makafiri. Hiyo ni dalili tosha kuwa mwezi huu ni kielelezo cha mgongano baina ya haki na batil.

Kinachowasibu ndugu zetu wawe wanachama wa Hizb ut Tahrir na Waislamu wengineo wengi walioko katika mahabusu si chochote bali ni katika gurudumu la mpambano huu baina ya haki na batil.

Kwa kuwa kwa uwazi usio na shaka, wengi wao hawana hatia, bali kosa lao kubwa  ni Uislamu, na ndio maana kinachotendwa ni kufanyiwa vitimbwi vya  hapa na pale katika kudhulumiwa kwa kisingizio cha ‘ushahidi haujakamilika’, ‘uchunguzi unahusisha nchi za nje’ nk. Waislamu na waadilifu katika wasiokuwa Waislamu wanajua udhati wa dhulma hiyo, na kamwe hawakubaliani na uwongo huo usioingia akilini uliombatana na chuki za wazi ambazo hazileti tija zaidi ya kuongeza mahusiano ya chuki na ya hatari ndani ya jamii, kwa kufanywa jamii fulani ina daraja duni inayostahiki kudhulumiwa, kudharauliwa na kudhalilishwa.

Tuchukue fursa hii kuwakumbusha tena kuwa kesi ya ndugu zetu wanachama wa Hizb ut Tahrir Tanzania, Ustadh Ramadhan Moshi, Waziri Suleiman na Omar Salum inatajwa tena leo tarehe 22 Mei 2018 katika Mahkama ya Wilaya- Mtwara mjini.

Wakati umefika kwa wasimamizi wa haki na sheria kuwaachia huru ndugu zetu hao, ili wakaendelee na maisha yao ya kawaida na familia zao,  kwa kuwa hawana hatia yoyote, na ndio maana mpaka leo, zaidi ya miezi sita sasa,  hakuna chochote kinachoendelea katika kuiendesha inayoitwa kesi.

Kwa upande mwengine, tuwaombe waadilifu katika Waislamu na wasiokuwa Waislamu wakemee dhulma hii ili kuirejesha jamii katika hali ya kuheshimiana na mshikamano.

Mwisho, tunawaomba Waislamu  haswa,  katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani wakithirishe kuwaombea dua ndugu zetu wote Waislamu watokane na mikono ya dhulma  na uonevu.

Tunamuomba Allah Taala kwa nguvu Zake awakomboe Waislamu wote katika uonevu na dhulma

 

Amiin

Afisi ya Habari –   Hizb ut- Tahrir Tanzania

06 Ramadhan 1439 Hijri   | 22-05-2018 Miladi

https://hizb.or.tz/

https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.