Waziri Suleiman Mkaliaganda: Aachiwe Huru, Apewe Dhamana Au Shauri Lake Lianze Kusikilizwa Mara Moja

بسم الله الرحمن الرحيم

Jina: Waziri Suleiman Mkaliaganda
Umri: 34
Kazi: Mwalimu wa Sekondari
Makaazi: Mtwara mjini
Mahala anaposhikiliwa: Gereza la Lilungu, Mtwara
Muda wa kuwa mahabusu: Karibu miaka 4 sasa
Alikamatwa tarehe 21/10/2017 karibu na nyumbani kwake mtaa wa Kiyangu, Mtwara mjini.
Kwa kipindi chote karibu mwezi na nusu Waziri Mkaliaganda alishikiliwa katika kituo cha Polisi Mtwara bila ya kupewa dhamana wala kupelekwa mahakamani.
Hatimae akabambikiziwa kesi ya ugaidi: PI NO. 9 OF 2017, na mnamo tarehe 5/12/2017 kimya kimya akaanza kupelekwa Mahkama ya Wilaya ya Mtwara kwa ajili ya kutajwa kesi yake.
Sasa ni karibu miaka 4 bado yupo kizuizini katika gereza la Lilungu, Mtwara huku kesi yake ikikosa ushahidi.
Waziri amekosa kuletwa mahkamani kwa mwaka mzima na miezi kadhaa mpaka hivi karibuni tarehe 20 Mei 2021 ndipo kesi yake imeanza kutajwa tena.
Mpaka sasa anaendelea kunyimwa haki zake msingi ikiwemo Magereza kuzuiya kupelekewa chakula, kutembelewa na familia nk.

Maoni hayajaruhusiwa.